Kafulila aliyekuwa Mbunge kinara
katika kuibua ufisadi wa sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 306 katika
akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), anakutana ‘uso
kwa uso’ na Jaji Utamwa, ambaye ndio alitoa hukumu tata iliyosababisha kuibuka
kwa kashfa ya ufisadi wa fedha hizo.
Jaji Utamwa aliitoa hukumu hiyo,
Septemba 8, 2013 kwa kumwamuru Kabidhi Wasihi, kukabidhi mtambo wa Kampuni ya
kufua umeme wa dharura ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwa mmiliki
wake mpya ambaye ni kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited
(PAP) baada ya kukubaliana na maombi ya aliyekuwa mbia wa IPTL, kampuni ya
Engineering and Marketing Limited (VIP) iliyoondoa kesi yake kwa lengo la
kuifilisi IPTL.
Hukumu hiyo ndio ilikuwa chanzo cha
Kafulila kuibua kashfa hiyo bungeni kwa kuwahusisha vigogo mbalimbali wa
serikali na ufisadi huo.