Hapa ni katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ibinzamata mjini Shinyanga.Pichani ni mabasi yaendayo mikoani.Leo Ijumaa Novemba 27,2015 saa mbili asubuhi askari wa kikosi cha usalama barabarani walitanda huku abiria na wananchi wakiwa na hamu ya kujua kulikoni!! Kumbe ni siku iliyopangwa kwa ajili ya Uzinduzi wa Kampeni inayoitwa "Abiria Paza Sauti".
MKUU wa kitengo cha usalama
barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro amesema kampeni hiyo
imeandaliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kupitia kikosi cha
usalama barabarani kwa kushirikiana na kushirikiana na taasisi isiyo ya
kiserikali inayoitwa Mabalozi wa usalama barabarani (Road Safety
Ambassador- RSA) pamoja na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini-
SUMATRA.
Mabasi
yaendayo mikoani yakiwa katika Stand ya Ibinzamata mjini Shinyanga leo
asubuhi-Uzinduzi wa kampeni ya "Abiria Paza Sauti" umefanywa na mkuu wa
kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro akiwa na
maafisa wa usalama barabarani kwa kutoa elimu kwa abiria wa mabasi ya
masafa marefu juu ya wajibu na haki zao wanapokuwa safarini .
Mkuu wa kitengo
cha usalama barabarani wilaya ya Shinyanga Vicent Msame akiwatangazia
abiria,madereva na wananchi wakiokuwa eneo la stendi ya Ibinzamata
kuhusu uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti
Maafisa hao wa polisi wakiwa na mkuu wao wa kitengo
cha usalama barabarani walipanda katika mabasi yaendayo mikoani kuanzia
kituo kikuu cha mabasi Ibinzamata mpaka Tinde huku wakitoa elimu kwa
abiria juu ya wajibu na haki ikiwemo kutoa taarifa wanapoona dereva yupo
katika mwendo kasi ambao siyo mzuri ili kunusuru maisha yao.
Kampeni
ya “Abiria Paza Sauti” ambayo ni endelevu ina lengo la kuwataka abiria
kupaza sauti katika kipindi cha mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka
ambacho huwa na abiria wengi unaosababisha madereva kuendesha kwa mwendo
kasi ili kufanya safari nyingi zaidi
Mabasi yakiendelea kuingia Stand
Maafisa wa usalama barabarani wakiwa eneo la stand,wakianza kuingia kwenye basi moja baada ya jingine
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiwa katika basi la Super Sami likitoka jijini Mwanza kwenda jijini Dar es salaam
Maafisa wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga wakitoa muongozo kwa madereva wa mabasi yaendayo mikoani
Mkuu wa kitengo
cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro akiwa katika basi
la Kisesa akitoa elimu kwa abiria ambapo amesema kampeni hiyo wameiandaa
kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayoitwa Mabalozi wa
usalama barabarani (Road Safety Ambassador- RSA) pamoja na mamlaka ya
usafiri wa nchi kavu na majini- SUMATRA.Kulia kwake ni mwandishi wa
habari wa Azam TV Stephen Wang'anyi akiwajibika
Mkuu huyo wa kitengo
cha usalama barabarani Chacha Maro amesema lengo la kampeni hiyo ni
kuwataka abiria wapaze sauti kwa kutoa taarifa zinazohatarisha maisha
yao wawapo safarini SUMATRA kwa kupiga simu namba 0800110019 au
0800110020 ,Trafiki makao makuu simu namba 0682887722 na kikosi cha
usalama barabarani,zoezi la kutoa elimu kwa abiria litakuwa endelevu
ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha abiria wanaosafiri kwa kutumia magari
madogo kuepuka kuwekwa nyuma ya gari(buti) kwani ni hatari kwa maisha
yao
Askari wa usalama barabarani wakijiandaa kupanda kwenye mabasi
WP Janeth Mkevela akitoa elimu kwa abiria waliokuwa wanasafiri na basi la Prince Isamilo kutoka Mwanza kwenda Moshi.Pamoja na mambo mengine aliwataka abiria kuwa jasiri kutoa taarifa wanapoona dereva anataka kuhatarisha maisha yao ,wafunge mikanda,kuhakikisha kuwa tiketi zao zina majina yao,namba za gari na siti,kufikishwa hadi mwisho wa safari yao,kudai nauli endapo chombo kitaharibika njiani na haki ya kupata huduma muhimu.
WP Janeth Mkevela akimhojia kondakta wa basi la Prince Isamilo kwanini tiketi ya abiria haina jina la abiria,namba ya gari na mahali anapokwenda
Abiria
wakiwa kwenye basi wakimsikiliza afisa wa kitengo cha usalama
barabarani.Abiria hao mbali na kushukuru kupewa elimu hiyo pia
waliliomba jeshi la polisi kuendelea na zoezi la kupima ulevi kwa
madereva ili kuhakikisha kuwa ajali zinapungua katika kipindi hiki cha
kuelekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Kulia ni Mwandishi wa habari gazeti la Nipashe na Malunde1 blog,bwana
Marco Maduhu akiteta jambo la afisa wa kitengo cha usalama barabarani
mkoa wa Shinyanga Janeth Mkevela baada ya kushuka kwenye mizani ya Tinde
Baadhi ya Maafisa wa kitengo cha usalama barabarani wakiwa katika mizani ya Tinde,kila basi lilikuwa na askari mmoja
Askari wa kitengo cha usalama barabarani Mohammed Nyagal akitoa elimu
kwa abiria wa basi la Zube Express juu ya wajibu na haki zao wawapo
safarini
Abiria wakiwa kwenye basi,kushoto ni bwana Victor Sango ambaye ni mdau
mkubwa wa Malunde1 blog akisikiliza elimu kuhusu kampeni ya Abiria Paza
Sauti
Askari wa kitengo cha usalama barabarani James Mgoha akitoa elimu kwa abiria juu ya wajibu na haki zao wawapo safarini
Abiria wakisikiliza elimu kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti
Hapa ni katika eneo la Mizani ya Tinde-Maafisa wa kitengo cha usalama
barabarani na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakijiandaa kurudi
Shinyanga mjini baada ya kumaliza zoezi la uzinduzi wa kampeni ya Abiria
Paza Sauti
Tunarudi mjini.....
Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga Chacha Maro akizungumza baada ya uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza sauti.
Amesema“Tumeanzisha
kampeni hii kwani katika kipindi cha mwisho wa mwaka huwa kuna abiria
wengi,matokeo yake madereva wakishirikiana na wamiliki wa vyombo vya
moto huendesha magari kwa mwendo kasi ili wawe na safari nyingi wapate
faida hali inayosababisha kutokea kwa ajali zinazogharimu maisha ya
wananchi”.