HATIMAYE mwanamuziki, Nguza Viking maarufu kama Babu
Seya na mwanae, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, wametua katika Mahakama ya Haki za
Binadamu Afrika
(AFCPHR) Arusha.
Wanamuziki
hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia
kifungo cha maisha gerezani.
Kupitia
shauri lao lililowasilishwa mahakamani na kupewa namba 006/ 2015, wanaiomba
Mahakama ya Afrika kutoa uamuzi kuwa haki zao zilivunjwa.
Kwa
sababu hiyo wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia.
Katika
shauri hilo pia wameomba wawezeshwe kupata msaada wa sheria na pia
wanataka Mahakama hiyo iteue wataalamu watakaotoa ufafanuzi wa hoja za
kesi yao na kuisaidia kufikia wajibu wake.
Miongoni
mwa hoja za walalamikaji hao zilizowasilishwa mahakamani hapo ni pamoja na
kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki.
Vilevile
wanadai hati ya mashtaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za
makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa kutayarisha utetezi
wao.
Pia
wanadai mahakama iliyowatia hatiani ilijielekeza katika
ushahidi wa upande wa mashtaka pekee usioshirikisha ushahidi mwingine.
Wanadai
kwamba Serikali ya Tanzania kupitia maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za
binadamu na sheria za kimataifa.
Wanadai
pia kwamba mlalamikiwa alivunja Ibara 1,2, 3, 5, 7(1)b), 13 na 18(1) ya Mkataba
wa Afrika kuhusu Ubindamu na Haki za Binadamu.Malalamiko
mingine ni kuwa baada ya kukamatwa hawakuelezwa mapema kuhusu mashtaka
waliyokuwa wakituhumiwa nayo.
Wanadai
kwa sababu hiyo waliwekwa chini ya ulinzi kwa siku nne bila kuwa na mawasiliano
na kupata fursa ya kuonana na mwanasheria au mtu mwingine ye yote.
Wanadai
wakiwa chini ya ulinzi polisi waliwatesa na kuwatukana na baadaye ofisa
mmoja wa polisi aliwaeleza kuwa wanatuhumiwa kwa ubakaji.
Walalamikaji
hao raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), walikuwa
wakiishi na kufanya kazi ya muziki Dar es Salaam.
Wanadai
kwamba mashtaka dhidi yao yalitungwa na hivyo hukumu iliyotolewa
haikujikita katika ushahidi wenye nguvu katika sheria.
Nguza
na wanawae watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa kituo cha
Polisi cha Magomeni Dar es Salaam.
Baadaye
walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16 mwaka
2003.
Watuhumiwa
hao pamoja na mwingine aliyejulikana kwa jina la Mwalimu walishtakiwa kwa
tuhuma 10 za ubakaji.
Pia
walikabiliwa na mashtaka 11 ya kunajisi watoto 10 wenye umri wa miaka
sita na nane. Watuhumiwa wote walikana mashitaka yao.
Baada
ya kusikilizwa kesi hiyo, Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam ilitoa hukumu
Juni 25, mwaka 2004.
Iliwatia
hatiani kwa kifungo cha maisha jela huku mtuhumiwa wa tano, Mwalimu
akiachiwa huru.
Walikata
rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania Oktoba 30 mwaka juzi ambako wafungwa
wawili Francis Nguza na Nguza Mbango walishinda rufaa yao.
Hata
hivyo, Babu Seya na Papii Kocha walijigonga mwamba na kurudishwa jela kwa
kuhukumiwa kifungo cha maisha.
JINSI
WALIVYOTIWA HATIANI
‘Babu
Seya’ na ‘Papii Kocha’ walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya
kupatikana na hatia ya ubakaji na kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi
Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.
Babu
Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto hao wa shule ya
msingi waliokuwa na umri kati ya miaka sita na minane.
Mahakama
iliwatia hatiani kwa makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri
huohuo kati ya Aprili na Oktoba 2003.
Juni
25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
aliwatia hatiani Babu Seya na wanae kwa hatia ya kubaka na
kulawiti.
Januari
27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo
alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi yao.
Hukumu
hiyo ilitolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Addy Lyamuya aliyewatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa
wameshitakiwa nayo Juni 25, mwaka 2004.
Awali
mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha
na wakili wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.
Mwaka
2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu
Februari 2010.
Mahakama
iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku
ikiwaachia huru watoto wake wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza.
Chanzo cha
habari ni gazeti la MTANZANIA.