![]() |
BASI la Simiyu Express likiwa eneo la tukio. |
ABIRIA
zaidi
ya sita waliokuwa wakisafiri na basi la Simiyu Express,ikitoka mkoani
Simiyu kuelekea Dar Es Salaam,inadaiwa wamepoteza maisha,baada ya basi
hilo walilokuwa kupata ajali mbaya jana
katika eneo la Chalinze Nyama mkoani Dodoma.
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa wetu aliyeko eneo la tukio anasema ajali hiyo
ilitokea mnamo majira ya saa moja usiku,huku akieleza chanzo cha ajali
ni kupasuka kwa tairi la mbele la basi hilo,lililosababisha gari hilo
kumshinda dreva na kwenda kugonga
mti aina ya mbuyu kisha kupinduka.
![]() | ||
Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa
katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu na
kwamba watu waliopoteza maisha ni wengi na majeruhi ni wengi.
