Kiungo wa Kimataifa wa Algeria, Yacine Brahimi(24) amekuwa raia wa kwanza wa Algeria
kutwaa Tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Afrika kwa 2014 kama
ilivyoendeshwa na Shirika la
Utangazaji la Uingereza (BBC).
Brahimi anayechezea Porto ya Ureno ametwaa tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura na washabiki wa soka,waliovunja rekodi ya upigaji kura kutoka nchi 207
zilizosajiliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Mwanasoka huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda kipa wa Timu ya Taifa ya Nigeria, Vincent
Enyeama; mchezaji wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, Gervinho na Yaya
Toure wote wawili wa Ivory Coast. Toure aliitwaa tuzo hiyo mwaka jana.
Baada ya kutwaa tuzo hiyo Brahimi alisema ni heshima kubwa kwake kupata tuzo hiyo ambayo ameamua kuitoa kwa ajili ya nchi yake na watu wote waliomchagua,
akisema pia kwamba ni kombe kwa watu wote wa Afrika.
Alisema kombe hilo litampa nguvu na ari ya kufanya kazi kwa bidii
zaidi, kuwa mzuri ndani na nje ya dimba ili aweze pamoja na timu
anazotumikia, kupata mafanikio makubwa. Msimu uliopita aling’ara sana
kwa klabu na nchi yake.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI