MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Kahama;Machibya Kidulamabambasi. |
SHIRIKA la HUHESO FOUNDATION la mjini
Kahama mkoani Shinyanga linatarajia kuwafikia watu 12,178 kwa lengo la
kuwawezesha elimu elimu juu ya kuanzisha vikundi vya kujiwekea kisha
kukopeshana fedha,ili kujiletea maendeleo katika familia zao na Taifa kwa
ujumla.
WASHIRIKI wa utambulisho wa Mradi wa Pesa kwa wote. |
Hayo
yalielezwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Juma Mwesigwa wakati akitambulisha Mradi
wa Pesa kwa Wote (PKW) kwa wakuu wa idara mbalimbali,maafisa watendaji wa kata
pamoja na maafisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri zote tatu
za wilaya ya Kahama,ambapo mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne.
MENEJA MRADI na Mkurugenzi wa Shirika la HUHESO FOUNDATION;Juma Mwesigwa akifafanua jambo. |
Mwesigwa alisema mradi huo umefadhiliwa na Cooperative for Assistannce and Relief Everywhere,inc,(CARE)in Tanzania ambao utatekelezwa katika mikoa saba hapa Tanzania ikiwemo Morogoro,Pemba na Unguja(Zanzibar)na mikoa ya kanda ya ziwa Mwanza,Tabora na Shinyanga.
Alisema kwa upande wa Shinyanga ni utatekelezwa katika wilaya za Shinyanga vijijini, Kishapu na Kahama.Ambapo kwa upande wa wilaya ya Kahama mradi huo utahusisha Halmashauri zote tatu Halmashauri ya mji wa Kahama,Msalala na Ushetu na Shirika lake litahusika na kuutekeleza.
“Lengo ni
kuwafikia watu 12,178 kwa miaka minne kwa Kahama, na tumepewa majukumu ya
kutekeleza mradi huo kwa kufadhiliwa m.45,206,500 kwa mwaka wa
kwanza ,na mkataba wake unanzia Octoba 01,2014 hadi Juni 30,2015.”Alisema
Mwesigwa.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la HUHESO FOUNDATION;Shija Felician. |
Hata hivyo mratibu wa mradi huo katika shirika hili,Fatuma Shabani naye alisema malengo ya mradi wa pesa kwa wote ni kuwajengea uwezo wanakikundi ili waweze kujiwekea akiba kwa malengo ya kuongeza uhakika wa kipato kupitia kujiwekea akiba zao, mfuko wa jamii na kutoa mikopo kwa wanachama kwa ajili ya maendeleo.
Alisema mradi huo utawafikia wanawake kwa asilimia70 na wanaume asilimia 30 ya idadi yote ya wanachama,kutoka katika jumla ya vikundi 487 kwa miaka yote minne katika Halmashauri zote tatu za Kahama kutoka kwenye kata 15 .
MMOJA wa washiriki katika Utambulisho huo,Afisa Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala;Aliadina Peter akitoa machango wake juu ya kuboresha Mradi wa Pesa Kwa Wote. |
Aliongeza
mradi huo utasaidia wananchi wa vijijini ambao kwa kiwango kikubwa kuna na
ukosefu wa huduma za kifedha,sambamba na ugumu wa masharti ya mikopo kutoka
Mashirika ya kifedha ambayo pia huwapa wakati mgumu wa kurejesha mikopo
kutokana na ukubwa wa riba jambo linalotoa wakati mgumu wa kufuata na kukamatiwa mali kwa
anayeshindwa kulipa.
“Tunautambulisha rasmi mradi wa pesa kwa wote na hilo ni jina tu siyo kwamba tunasambaza pesa,Shirika hili litawajengea uwezo wanakikundi ili waweze kukopeshana wenyewe,ambapo tutawahamasisisha kwa kufanya mikutano ya hadhara kupitia Watendaji wa kata na vijiji hadi mitaa,ili wamudu kuunda vikundi vya kukopeshana wenyewe kwa masharti nafuu,”Alisema bi Fatuma.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri mji wa Kahama,Machibya Kidulamabambasi akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo,Benson Mpesya aliwataka shirika hilo kufanya kile walichokusudia na mradi huo usiishie mikononi mwa watu wachache kwani fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili huwa haziwapati walengwa.
“Kwaniaba ya Serikali niwaombe mwendelee kushilikiana na idara za Halmashauri ya mji wa Kahama pamoja na kuwatumia maafisa maendeleo kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi kuhusu mradi huo wa pesa kwa wote,”
DIWANI wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CCM,Josephine Baranoga naye akitoa mchango wake. |
Aliongeza;“ Kusudi mfadhili aendelee kusaidia
wananchi lazima mjitume,msiwe kama mashirika mengine ambayo yamekuwa
yakijinufaisha kupitia miradi mbalimbali inayotolewa na wafadhili, sisi kama
halmashauri hatutaki kusikia ubabaishaji huo unatokea, nawashauri watu wajiunge
makundi ili wapate mafunzo hayo iwe njia rahisi ya kukopeshana.”
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI