BEKI wa kati
wa Malaga,Welgton amedai aliitwa mtoto wa Kahaba na mshambuliaji,Lionel Messi
hiyo ndio sababu
ya kumshika mdomo wake na kumsukuma chini.
Kikosi cha Malaga
kinachonolewa na Javi Gracia,kilikuwa cha kwanza katika msimu wa 2014 – 15
kuwadhibiti Barcelona kiasi cha kutoshana nguvu,na washindi wa pili wa La Liga
kushindwa kupiga hata shuti moja langoni mwa Maliga.
Katika mchezo huo ghafla Weligton alionekana kumshika mdomo Messi,ambaye alianguka na wachezaji wa Barca kumshawishi mwamuzi amtoe nyota huyo raia wa nchini Brazil kwa kadi nyekundu,lakini alionyeshwa kadi ya njano.
Kocha huyo alikiri
kumficha Messi kuliua makali ya timu yake ambayo ilikosa uelekeo kiasi cha
kumaliza dakika tisini pasipo kupiga hata shuti moja langoni kwa wapinzani wao.