IMEELEZWA kwamba ifikapo mwaka 2030, kuna uwezekano mkubwa wa
kudhibitiwa kwa Janga la Ukimwi duniani,hii
ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la kupambana na Ukimwi.
Shirika hilo linasema idadi ya maambukizi mapya na wanaokufa
kutokana na Ukimwi
imeendelea kushuka.
Shirika hilo linasema idadi ya maambukizi mapya na wanaokufa
Hata hivyo jitihada zaidi za kimataifa zinahitajika kwani zilizopo hazitoshi kumaliza janga hilo.
shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres limeonya kuwa watu wanaoishi na virusi hivyo hawapati dawa za kutosha.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa watu milioni 35 duniani wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa maambukizi mapya milioni 2.1 yalitokea mwaka 2013. Idadi hii iko chini kwa asilimia 38 ikilinganishwa na mwaka 2001.
Vifo kutokana na HIV pia vimepungua kwa asilimia 5 katika miaka mitatu iliyopita. Kwa sasa watu milioni 1.5 hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI