Sunday, October 10, 2010

KITUO CHA MAFUTA CHATEKETEA MOTO KAHAMA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

KITUO CHA MAFUTA CHATEKETEA MOTO KAHAMA.

KITUO cha mafuta cha Takukulu Filling Station kilicho kitongoji cha Nyakato wilayani Kahama kimeteketea moto na kusababisha hasara ya zaidi ya Shilingi Milioni 276 na kusababisha hofu kubwa kwa wakazi wa mji wa Kahama ambao wamefikia hatua ya kuiomba Serikali ivihamishe vituo vilivyo kati ya makazi ya watu.
Tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa majira ya saa kumi jioni na kuteketeza Lita Elfu sabini za mafuta aina ya Petroli sambamba na gari aina ya Volvo kampuni ya Camel lililokuwa likishusha mafuta katika kiytuo hicho,huku gari la zimamoto la Halmashauri likishindwa kudhibiti ajali hiyo kutokana na kutokuwa na wataalamu sambamba na kufika eneo hilo likiwa na maji pungufu.

Kufuatia gari hilo kufika eneo hilo pasipo kuwa na wataalamu huku likiwa na maji pungufu,baadhi ya watu waliokuwa katika eneo hilo la tukio walishikwa na jazba na kumshushia kipigo aliyekuwa kiongozi wa shughuli za kuzima moto kupitia gari hilo hadi pale lilipofika gari kutoka mgodi wa Buzwagi ili kuuzima moto huo.
Aidha wakazi wa mji wa Kahama ambao waliingia na hofu kutoka na mazingira ya tukio hilo huku wakifedheheshwa na gari la zimamoto la Halmashauri kutokuwa na wataalamu wameiomba Serikali Wilayani hapa kuhakikisha kuwa vituo vyote vya mafuta vinatolewa katika eneo la katikati mji na kuwekwa nje ya Mji ili kepuka majanga ya moto yanayoweza kutokea. 



Hata hivyo katika haloi ya kustaajabisha wakati moto kubwa ukiendelea kuwaka eneo hilo baadhi ya watu wanaosadikiwa wanaishi eneo hilo walikuwa wakifanya vitendo vya uhalifu wa wizi wa bidhaa mbalimbali yakiwemo mafuta pamoja na vifaa vya kuzimia moto kutoka katika gari la Mgodi wa Buzwagi.
Akisimulia tukio hilo Meneja wa Kituo hicho;Donald Cosmas [37] ambaye aliunguzwa miguu yake na mvuke wa moto alisema chanzo cha tatizo hilo huenda kimetokana na shoti ya betri ya gari ya gari hilo la Volvo lililokuwa likishusha mzigo wa mafuta kutokana na tingo wake kuwa akijishughulisha na sehemu hiyo ya betri.

Wakazi hao wakiongea na Mwandishi wa Habari hizi walisema kuwa katika mji wa Kahama kuna vituo vitano vya mafuta ambavyo vipo katikati ya mji hali ambayo ni hatari kwa usalama wa wakazi hao pindi janga kama hilo likitokea na kuomba uongozi wa wilaya kuona umuhimu wa kukinga janga hilo kuliko kusubiria tiba.

Kufuatia kuungua kwa kituo hicho baadhi ya Wakazi hao walilaani vitendo vilivyofanywa na Wananchi waishio katika eneo hilo kwa kufanya vitendo vya wizi katika gari la zimamoto likuwa kizima moto kutoka katika Mgodi wa Buzwagi kwa kuiba baadhi ya vitu vikiwemo vifaa vya kuzimia moto hali iliyopekea gari hilo kuacha zoezi hilo na kurudi mgodini.

Walivitaja baadhi ya Vituo hivyo vya mafuta kuwa ni Jamco Filling Station, Kahama Filing Station, Samanga filing Station ambayo vipo katikati ya Mji huku vikizungukwa na makazi ya watu hali ambayo ni hatari kwa usalama wao.

Hata hivyo katika tukio hilo la kuungua kwa kituo hicho cha mafuta cha Kakukulu akukuwa na madhara yeyote yaliotokea mbali na Mtoto mmoja ambayo 
hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana kuvunjika mkono katika jitihada za kukimbia baada ya tangi la Mafuta kulipuka

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Meja Mstaafu Bahati Matala alipotafutwa kuzungumzia juu ya tukio hilo hakuweza kupatikana kutokana na kwa sasa kushikilia Wilaya mbili kiuongozi za Bukombe na Kahama.

Polisi wilayani Kahama imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kulaani vikali watu waliofanya uhalifu wa wizi na kusema imeandaa mikakati mikubwa ya kuwasaka ili hatua kali za kisheria dhidi yao ichukuliwe

Mwisho

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI