Thursday, September 21, 2017

SERIKALI YATANGAZA AJIRA ZA WALIMU KWA SHULE ZA MSINGI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

S
erikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza ajira za Walimu wa Shule za Msingi Nchini.

 

Ajira hizo zimetangazwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zinahusisha walimu ambao wamemaliza masomo yao mwaka 2014/2015 katika ngazi ya cheti (III A).
 

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kuthibitishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa walimu ambao wamemaliza mwaka 2014/2015 na walituma maombi yao kwenye tangazo la kazi ya Agust 10, 2017 hawatakiwa kuomba upya kwani barua zao zinafanyiwa kazi.
 

Kufuatia tangazo hilo la ajira,litasaidia kupunguza ombwe linaloikabili Serikali la upungufu wa Waalimu nchini,hatua ambayo pengine itaanza kutoa muelekeo wa uboreshaji wa elimu nchini.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI