Saturday, September 23, 2017

MUME ACHOMWA KISU KWA KUMDHIBITI MKEWE KUJIRUSHA KATIKA STAREHE

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



M
aria Mwanahiya mkazi wa  kijiji cha Ntatumbila  wilaya Nkasi mkoani Rukwa amemjeruhi vibaya
mume wake kwa kumchoma kisu ubavuni,baada ya kudhibitiwa na mumewe kujitanua katika masuala ya anasa.


Kitendo hicho kimedaiwa kumtia hasira,Maria kutokana na kutofurahishwa kiasi cha kukereka,kutokana na mume wake kumlazimisha kuacha starehe zake ikiwemo kunywa pombe.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 10:30 usiku katika kijiji cha Ntatumbila  wilaya Nkasi mkoani Rukwa muda mfupi baada ya mwanamke huyo kurejea nyumbani kutoka kilabuni alipokuwa anakunywa pombe. 
Inaelezwa kuwa mwanaume huyo aliporudi nyumbani kwake kutoka katika shughuli zake hakumkuta mke wake na wala mke hakuweka chakula kwa ajili ya mmewe hali iliyomlazimu kumfuata mkewe kwenye kilabu ya pombe.
Alipofika kilabuni, alimlazimsha mkewe kurudi nyumbani lakini mwanamke huyo aligoma,hata hivyo baadhi ya watu waliokuwa wanakunywa naye pombe walimsihi arudi nyumbani, ndipo alipokubali kwa shingo upande akarudi na mmewe.
Baada ya kufika nyumbani ulizuka ugomvi mkubwa wa kurushiana maneno kati ya wanandoa hao ambapo mwanamke huyo alikuwa akimwambia mumewe aache kumfuata fuata anapokuwa kwenye starehe zake  kwani yeye siyo mtumishi wa nyumbani.
Wakati wakiendelea kufokezana kwa muda mrefu, ndipo mwanamke huyo alipoamua kwenda jikoni kuchukua kisu na kumchoma mumewe ubavuni na kumsababishia jeraha kubwa ambalo lilivuja damu nyingi.
Tukio hilo lilisababisha watu kujazana katika nyumba yao na kuamua kumkamata  mwanamke huyo na kumpeleka kituo cha polisi na mume wake  kumkimbiza hospitalini ili akapatiwe matibabu ili kuokoa maisha yake.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ntatumbila Daniel Kalumbilo amesema hilo ni tukio la pili kwa mwanamke huyo kumshambulia  mumewe kwa silaha za jadi ambapo aliwahi kumpiga mpini  na kumuumiza kichwa mpaka akafanyiwa upasuaji.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwasihi wanandoa kujitahidi kutatua migogoro yao kwa njia ya amani na iwapo wanashindwa wawashirikishe ndugu wengine kuliko kupigana na kuumizana. 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI