Thursday, August 17, 2017

MAUAJI YA KISHIRIKIANA,UTUPAJI VICHANGA KUTOKOMEZWA NA ELIMU.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




M
atukio ya mauaji ya dhidi ya Vikongwe,watu wenye ualibino vinavyosadikiwa
kusababishwa na imani za kishirikina,kutokomezwa pindi jamii itakapowekeza katika suala zima la elimu.



Mbali na matukio hayo,jamii ikielimika itakuwa nyenzo muhimu ya kutokomeza vitendo vya kinyama vilivyokithiri vya kutupa watoto wachanga mara wanapozaliwa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Rocken Hill Academy,inayomiliki shule za Msingi na Sekondari wilayani Kahama,Alexander Kazimil,amebainisha hayo katika mahafari ya 13 kwa shule za msingi zilizo katika taasisi yake.

Ameisitiza katika dunia ya Utandawazi,elimu ni nyenzo muhimu katika kustawisha familia na taifa,hivyo ni vyema jamii ikatumia nguvu nyingi katika kuhakikisha rasilimali pekee wanayowekeza kwa ajili ya vijana wao,inakuwa elimu.

Kazimil alisema jamii nyingi nchini bado  imeendelea na matukio ya mauaji yatokanayo na ushirikina kwa vikongwe na albino huku vichanga vikitelekezwa kwa kutupwa baada ya kuzaliwa kutokana na kukabiliwa na ombwe la kutoelimika.

“…naamini kupitia elimu,jamii itaimarika kiuchumi na kuondokana na vitendo hivyo viovu,hivyo nasisitiza sana wazazi wekezeni kwa watoto wenu elimu,kwani ndio silaha ya kupinga maovu,”anasema Kazimil.

Anaendela kusisitiza katika kipindi hiki cha upepo mkali wa Utandawazi,taifa litafikia malengo yake ya kuwa na viwanda huku jamii yake ikiwa na uchumi wa kati pindi uwekezaji katika elimu ukipewa kipaumbele,hasa kwakuwa Serikali imetoa fursa pana ya utoaji elimu bure kuanzia chekechea hadi darasa la kumi na mbili.

Aidha alisema ili kujenga taifa lenye watumishi wazalendo,ni budi wazazi na taasisi za elimu zikashirikiana katika kuhakikisha linawalea vijana katika maadili mema,yatakayowafanya kuondokana na tama ya mafanikio ya haraka,ambayo yamekuwa kichocheo cha kuwepo kwa vitendo vya rushwa na ufisadi.

Awali Meneja wa Shule za Msingi za Rocken Hill Academy na Rocken Hill Junior,Ephraim Kabeya,aliiomba jamii kutoa ushirikiano wa kimalezi kwa vijana na taasisi za kielimu kusudi zimudu kutoa vijana watakaokuwa viongozi imara na wenye maono ya kuipasha nchi kiuchumi.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga,Said Pamuyi,aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafari hayo,alisema ili jamii ipate mafanikio ni vyema wazazi na walezi wkawajenga vijana wao katika maono sahihi ya kiuchumi na kuwasimamia vyema katika maadili.




KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI