
W
|
aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa tume huru aliyoiunda juu ya
ufumbuzi wa utata uliojitokeza wa idadi ya watoto mapacha.
Taarifa hiyo ilitokana na uchunguzi baada ya
kujitokeza malalamiko ya Bi. Asma Juma
kuhusu kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya
Temeke Dar es salaam.

“Nimepokea taarifa kutoka kwa tume
huru niliyoiunda hivi karibuni na imethibitisha kuwa Bi. Asma Juma
hakuwa na watoto mapacha ila uchukuaji mbaya wa picha ya mtoto aliyekuwa
tumboni uliofanywa katika zahanati ya Huruma ukatoa matokeo hayo”
alisema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa
kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Bi. Asma aliamini hivyo kwa
sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali
walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Aidha Dkt. Majige Amesema kuwa
tume hiyo imebaini kuwa Bi. Asma hakuibiwa mtoto na alikua hana mapacha
kwa sababu uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika
chumba cha upasuaji kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.
Kwa upande wake mwakilishi wa
Familia ya Bi. Asma Juma Jordan Jaddah amesema kuwa anaishukuru Serikali
kupitia Wizara ya Afya kufatilia jambo hilo kwa ukaribu na kupata
ukweli wa malalamiko yao na wameikubali taarifa hiyo .
“Tunaipongeza tume hiyo chini ya
Wizara ya Afya na tunashukuru kwa msaada wao mwanzo mpaka mwisho na
kutupatioa majibu ya kuridhisha nasi tutakuwa bega kwa bega katika
kumfariji ndugu yetu kwa jambo hili lilitokea” alisema Bw. Jaddah.
Mbali na hayo Waziri Ummy
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa maagizo ya kila mtoto wa kike atakaepata ujauzito shuleni
asirudi shuleni ila aendelee na masomo mengine ya ujuzi.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI