
R
|
ais wa Serikali wa awamu ya tano ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,anatarajiwa kufungua
Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam,Julai Mosi mwaka huu.
Rais atafanya ufunguzi huo katika
Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam,kwa
kufungua maonesho hayo yanayotambulika kama maadhimisho ya Sabasaba.
Kwa mujibu wa taarifa kwa Vyombo vya Habari
iliyotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,ameeleza lengo la maonesho ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani
na nje ya nchi, pamoja na taasisi mbalimbali kujitangaza huduma na biashara wafanyazo.
Amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wafanyabisashara wa ndani kujifunza mambo ya
biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa,
kutengeneza mitandao ya mawasiliano baina yao ambayo itasaidia kukuza
biashara na kufikia malengo waliyojiwekeka na pia kutoa fursa ya kuuza
bidhaa.
“Maonesho haya yanabeba kauli mbiu
isemayo Ukuzaji wa Biasha kwa Maendeleo ya Viwanda, inanalenga kutumia
Maonesho haya kama jukwaa la kutangaza biashara na huduma mbalimbali kwa
ajili ya ukuzaji wa sekta ya viwanda, ikizingatiwa kuwa Serikali ya
Awamu ya Tano inaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza uchumi wa viwada
hapa nchini,”ilisema taarifa ya Waziri.
Aidha Maonesho ya mwaka huu yatatoa
fursa kwa wenye viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kukutana na wanunuzi
wa bidhaa zao na kutakuwa na kampeni maalum ya kuhamasisha wananchi
kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
“Napenda kuwafahamisha kuwa Tan
Trade kwa kushirikiana na washirika wake kwa mara ya kwanza imeandaa
Siku ya ‘Afrika Mashariki’ ambayo itaadhimishwa tarehe 6 Julai, 2017.
Lengo la siku hii ni kuimarisha biashara katika nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Kama inavyojulikana nchi hizi zimejaliwa kuwa na
rasilimali nyingi hali ambayo itatoa fursa nzuri katika maendeleo ya
kiuchumi katika nchi hizo ili kuwe na uchumi endelevu,” ilisema taarifa hiyo.
Katika maonesho hayo, Waziri anaeleza
kuwa Tan Trade imeandaa eneo maalum litakalojulikana kwa jina la ‘Banda
la Tanzania’ kwa ajili ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali
zinazotengenzezwa ndani ya nchi na ‘Banda la Asali’ kwa ajili ya kukuza
bidhaa za nyuki.
Pia kutakuwa na eneo maalum la wazalishaji wa bidhaa
za ngozi ambalo washiriki wake watapata fursa ya kuonesha bidhaa bora za
ngozi kwa ajili ya kuvutia wananchi wengi kupenda bidhaa zinazozalishwa
hapa nchini.
Katika kuimarisha huhusiano wa
kibishara na kuwakutanisha wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao
kutoka nje ya nchi, kutakuwa na banda maalum kwa ajili ya mikutano ya
kibiashara yaani Business to Business (B2B) na pia banda maalum
litakalotumika kwa utoaji wa mafunzo ya kibiashara.
Hadi sasa washiriki zaidi ya 2500
kutoka ndani na nje ya Afrika wamethibitisha kushiriki Maonesho ya mwaka
huu. Nchi zitakazoshiriki ni Burundi, China, Comoro, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Misri, Ujerumani, Ghana, India, Indonesia,
Iran, Italia, Japan, Kenya, Malawi na Mauritius.
Nchi zingine ni pamoja na Morocco,
Msumbiji, Namibia, Pakistani, Rwanda, Singapore, Afrika Kusini, Sudani
Kusini, Syria, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Uganda,
Marekani, Uingereza na Vietnam.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI