R
ais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ,Dk.John Magufuli ,ameiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha inatoa kiasi
cha Shilingi Bilioni 1.3,ndani ya
siku saba,ili zitumike kununua madawa ya
kudhibiti kuzaliana kwa mbu,wanaohatarisha uhai wa Watanzania kwa kuambukiza
maradhi mbalimbali,ikiwemo homa ya Malaria.
Imeelezwa kwamba kuna zaidi
ya lita 100,000 za madawa ya viatilifu vya viuadudu vya mazalia ya mbu
,zilizokosa soko katika kiwanda cha Biotech Products Limited,kilichopo Mji
Wa Kibaha ,Pwani,ambazo zingenunuliwa na Halmashauri mbalimbali nchini
zingesaidia kudhibiti kuzaliana kwa wadudu hao hatari kwa afya ya Binadamu .
Aidha ameeleza agizo hilo litaenda pamoja na maelekezo atakayoyatoa kwa kila halmashauri ikatwe kiasi gani katika fedha hizo .
Dk.Magufuli
amewataka wakurugenzi wa halmashauri nchini kila mmoja aanze kupanga
ratiba yake ya kwenda kuchukua akiba yake ya madawa ambayo yatakuwa
kwenye utaratibu kwa kila halmashauri .
Amekitaka
pia kiwanda hicho kijitangaze katika vyombo mbalimbali vya habari na
kutoa elimu kwa jamii kuwa madawa hayo hayana madhara kwa matumizi ya
binadamu .
Hayo
aliyasema ,wakati alipokwenda kutembelea kiwanda cha kuzalisha
viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria cha Tanzania Biotech
Products Limited katika ziara yake ya kikazi ya siku ya tatu mkoani
Pwani ,ambapo ni hatima ya ziara hiyo .
Anasema
kiwanda hicho tangu kifunguliwe na rais mstaafu Wa awamu ya nne
dk.Jakaya Kikwete dawa zinatengenezwa na kujazana bila kununuliwa .
Dk.Magufuli
,alieleza kuwa ,serikali inatumia mabilioni ya fedha kununua madawa
ikiwa ni pamoja na mwaka 2015 serikali ilitenga bil. 31 na mwaka 2016 na
2017 serikali imetenga bil.250 .
""Mzalishe
na kufanyakazi zenu, pasipo kuchakachua ubora uliopo ,kisa kupata soko
,nataka nione ugonjwa wa malaria unamalizika baada ya muda na wagonjwa
wanapungua mahospitalini " alisema dk .Magufuli .
Alieleza lengo kuu ni kuondoa ugonjwa Wa malaria kama ilivyo Zanzibar .
Dk .Magufuli ,alisema wananchi wanapaswa wanunue madawa hayo ili kujikinga na kumaliza ugonjwa huo ,hapa nchini.
Alibainisha
kwamba ,ni maajabu nchi za nje na Niger ,wananunua madawa hayo nchini
Tanzania huku watanzania kushindwa kununua bidhaa zinazozalishwa hapa.
Nae
kaimu Mkurugenzi wa Kiwanda hicho,Samwel Mziray ,alisema halmashauri
nyingi bado hazijanunua dawa hizo ili kutimiza malengo ya serikali .
Mziray
alisema awali ilielekezwa madawa yanayozalishwa ilikuwa ni jukumu la
wizara ya afya kuzinunua kisha kuzisambaza kwenye halmashauri nchini
ambapo ilijiengua .
"Tatizo hapa ni oda ,tukitengeneza madawa mengi yana muda ,inatakiwa yakishazalishwa yatumike ili kuzalisha mengine " alisema .
Mziray ,alisema kwasasa wanazalisha lita 48,000 za dawa kwa wiki na kuuza kwa sh .13,000 kwa lita .