Tuesday, June 27, 2017

YATIMA WANA UMUHIMU KATIKA JAMII

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



M
eya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda,amesherehekea sikukuu ya kumaliza mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani,kwa kupata chakula cha

pamoja na watoto yatima,huku akiikumbusha jamii umuhimu wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Aidha amewataka wananchi, taasisi  na viongozi mbalimbali wenye uwezo kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira

  magumu kwa lengo la kuwakwamua na hali ya kiuchumi iliyopo kwa sasa.

Mwenda ameyasema hayo Jijini Dar es salaam jana katika hafla ya Idd aliyoindaa nyumbani kwake na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni.

Alisema pamoja na mambo mengine,kufanya hivyo ni kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika harakati zake za kimaendeleo anazozifanya.

Alisema viongozi wananchi pamoja na jamii kwa ujumla haina budi kuendana na dhamira aliyonayo Rais Magufuli ya Taifa kujikwamua kiuchumi hususani kipindi hiki anapofanya mambo mbalimbali ya kuliletea maendeleo.


 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akizungumza wakati wa  hafla ya Idd aliyoindaa  nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. na kusheherekea na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .

 Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada.

 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi  watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha  Umra kilichopo Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni .baadhi ya zawadi aliyowaandalia (kushoto) Mratibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Imra James Gabon.

 Mke wa Meya Mama Tausi Yusufu Mwenda (mwenye nguo ya bluu) akimkabidhi moja ya zawadi Bi.Nuhimu Iddi anayetoka katika kituo hicho.

 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Yusufu Mwenda akiwakabidhi zawadi watoto

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI