TISHIO
la watoto kuliwa na fisi wanapokwenda shuleni katika kijiji cha
Busulwangiri,Kata ya Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala,wilaya ya
Kahama,Mkoani Shinyanga,limesababisha kufanyika hamasa ya kujenga
shule,kuwanusuru vijana wao kukumbwa na kdhia hiyo.
Hamasa
hiyo imefanywa na Wananchi wa kitongoji cha Kolandoto,kijijini Busulwangiri
katika Kata ya Bulyanhulu,ambao miongoni mwao,watoto wao waliishaliwa na fisi,wakati
wakienda shule iliyo mbali na eneo wanaloishi,anaandika Paschal Malulu.
Maamuzi
ya wananchi wa kitongoji hicho,kujenga shule kwa kujitolea ili kunusuru watoto
wao kuliwa na fisi,kutokana na umbali uliopo kwenda kwenye shuleni, ambayo ili
kuifikia,kuna msitu mkubwa unaokaliwa na wanyama hao hatari kwa maisha ya
binadamu.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Busulwangiri,Joram Kudisa,alisema kitongoji hicho cha Kolandoto,kiko
umbali wa kilometa 12 kufika katika eneo la shule ya msingi Busulwangiri,hivyo
kusababisha kuwepo kwa matukio ya watoto kuliwa na fisi.
Baada
ya kukithiri kwa matukio hayo ya watoto kuliwa na fisi,wazazi katika Kata hiyo
walianzisha utamaduni uliowalazimisha kila siku asubuhi kuwavusha watoto wao
wadogo katika eneo hilo la msitu,ili kuwalinda wasiliwe na mnyama huyo.
Mwenyekiti
huyo alieleza hayo mbele ya ujumbe kutoka mradi wa kuboresha elimu Tanzania
Equip ambao ulitembelea kijiji hicho kuona juhudi zinazofanywa na wananchi hao
kuboresha elimu na kuongeza tija kwa watoto wadogo kwenda shule baada ya kuanza
ujenzi wa shule katika eneo hilo
Alisema
kwa kuanza wamejenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ambayo
itatumika kwa masomo ya awali na darasa la kwanza na la pili,kwa ajili ya watoto
wenye umri wa miaka minne hadi saba,ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakisoma
kwenye mazingira magumu na hatarishi.
Anasema;“…hasa
wakati wakienda shule ambapo mara nyingi hufukuzwa na fisi kwa lengo la kuliwa
tofauti na wale watoto wakubwa ambao wanauwezo wa kukimbia”.
Kudisa
alibainisha kwamba kwa kuanza shule hiyo itakuwa na watoto wenye umri huo
85,ambapo tayari kaya 96 kutoka kitongoji hicho, zimechangia ujenzi huo.
Afisa
Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohamed Kahundi.alisema serikali itafanya jitihada za
kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika mapema na kuanza kazi,huku akichangia
Shilingi Laki Moja,kuwaunga mkono wanakijiji hao ambao tayari walikwisha kuchanga
Shilingi Laki Tisa.
Hata
hivyo Kahundi aliwakumbusha kwamba pamoja na juhudi hizo,ni budi shule hiyo iwe
na vyoo,pasipo kujali idadi ya vyumba va madarasa,kwa kuhadharisha kuwa
hata kama shule ingekuwa na vyumba 10 bila kuwa na choo haiwezi
kufunguliwa.
Alisisitiza
serikali haitakuwa taari kuifungua shule ikiwa na mazingira ya hatari kama hayo,
na kuongeza kuwa shule haiwezi kuanza bila kuwa na choo,na kutaka suala hilo
lipewe kipaumbele,ndipo kwa kutumia mamlaka yake ya afisa elimu mkoa atahakikisha analeta walimu
mapema iwezekanavyo, ili iweze kuanza mapema.
Kwa
pande wake mwakilishi wa Equip Tanzania Victoria Mushi alisema mradi huo
umekuwa ukitoa ushirikiano mkubwa katika jamii kuhakikisha vinapatikana vituo
vingi vya watoto kupata elimu zikiwemo huduma kama vile maji shuleni hali
ambayo kuhamasisha watoto kupenda kwenda shule kutokana na mazingira hayo
ya kusomea kuboreshwa na kuwa rafiki kwa wanafunzi hao.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI