JESHI
la Polisi limedhibiti mkutano mkuu maalumu wa Chama cha Wananchi “CUF”ambao
ungehudhuriwa na
Katibu Mkuu wa chama
hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mjini Tanga.
Jeshi
hilo likidhibiti mkutano huo jana,limeshiriki kikamilifu kumlinda Mwenyekiti
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba,wakati
akifanya usafi soko la Buguruni.
Lipumba
aliungana na Watanzania katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli,kufanya kazi ya usafi,inayotekelezeka siku
ya Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi.
Kitendo
hicho cha Mwenyekiti huyo anayetambulika na Msajiri wa Vyama vya
Siasa,kimetetewa na Msemaji wa CUF,wa
kambi inayomkubali Profesa Lipumba,Abdul Kambaya,kwa kusema hakuna jambo la
ajabu, kwa Kiongozi wa Chama cha Upinzani,kufanya usafi huku akilindwa.
Wakati
Lipumba akiunga jitihada za Rais Magufuli kwa kuwepo utamaduni wa kusafisha
mazingira,chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi,mapema jana, polisi mjini Tanga
ilizuia mkutano uliopangwa kuhudhuriwa na Maalim Seif.
Katika
mkutano huo ambao ulikuwa na agenda ya kujadili madiwani 12, waliopigana wiki
iliyopita katika ofisi za chama hicho wilayani humo, baada ya kugawanyika
kuhusu uamuzi wa wenzao kuhudhuria baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba 12.
Taarifa
ya jeshi hilo ilidai kuzuiwa kwa mkutano huo ni kutokana na tisho la uvunjifu wa
amani na kuwapo kwa makundi mawili yanayozozana. Mkutano huo ulipangwa
kufanyika katika Hoteli ya Mkonge mjini Tanga.
Pia,
taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga, Idd Abdallah ilisema
ukumbi ambao mkutano huo ungefanyika ni mdogo kutokana na wingi wa wanachama.
“Ukumbi uliopangwa kufanyika kwa mkutano huo
ni mdogo na ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mkutano wa chama hicho ngazi ya
wilaya ulivunjika kutokana na vurugu,” alisema
Akizungumzia
sakata hilo, Mwenyekiti wa CUF wa wilaya hiyo, Rashid Jumbe alisema hata kama
jeshi hilo limezuia mkutano huo, lengo la chama kuwajadili madiwani hao liko
palepale.
Alisema
kamati ya utendaji imependekeza madiwani saba,kati ya 12 wafukuzwe uanachama
kutokana na kukiuka msimamo wa chama,huku watano wakibaki chini ya uchunguzi.
Amebainisha kwamba katika fagio hilo,Mbunge (Mussa
Mbaruku),hatasalimika kwani alishiriki kikamilifu,pamoja na Naibu Meya (Mohamed
Aniu).
“…. kwa sasa tunafanya utaratibu na jeshi la polisi
kutekeleza masharti na vigezo wanavyotaka ili kuufanya mkutano huo tena,” alisema.