KAMPUNI
ya Bakhresa Foods imedhamiria kutekeleza kwa vitendo ahadi ya serikali ya awamu ya tano ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati,kwa ujenzi wa viwanda maeneo kadhaa hapa nchini.
Dhamira hiyo ambayo itatoa mchango mkubwa wa ajira nchini,na kukuza uchumi ni kuongeza viwanda vingine vya usindikaji
matunda hapa nchini ili kuongeza thamani kwa mazao ya wakulima.
Ahadi
hiyo imetolewa Jumanne,tarehe 11 Oktoba, 2016 na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo,Said S. Bakhersa, wakati alipokutana na Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ofisini kwake Magogoni,
jijini Dar es Salaam.
Bakhresa amesema wana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya
Kanda ya Ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa watu
wanapata usumbufu wa kusafirisha matunda hadi Dar es Salaam ndipo
wayauze.
Anasema Kuanzia
tarehe 15 Oktoba,mwaka huu wataanza kupokea matunda kutoka wilayani Kahama na maeneo ya
jirani,ambapo matarajio kwa siku watapata semi trela zaidi ya 30.Kisha wanatarajia kupokea tena kutoka mikoa ya Pwani na Kusini.
Anasema;“Tukijenga
kiwanda Kanda ya Ziwa, tutapunguza adha ya wadau kusafirisha matunda
kutoka kule hadi hapa kiwandani na badala yake sisi tutakuwa
tunasafirisha concentrated juice na kuileta hapa kwa hatua zaidi za
usindikaji.”
Aidha anasema
wana mpango wa kuendeleza usindikaji wa vyakula vya nafaka kwenye mikoa
ya Kusini na kwamba hadi sasa wameajiri wafanyakazi zaidi ya 8,000
wakiwemo Watanzania 180 ambao wameajiriwa kwenye matawi yake nje ya
nchi.
“....hawa tunawalipa kama expatriates,” anasema.
Amefafanua kwamba kwa
hivi sasa Kampuni hiyo imekwishafungua matawi mengine kwenye nchi za
Rwanda, Burundi, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini.
Kampuni
ya Bakhresa Foods inatengeneza vyakula mbalimbali zikiwemo juisi, soda,
maji, biskuti, ice-cream, vyakula vya nafaka kama ngano, mahindi,
mchele na bidhaa za kuokwa.
Kwa
upande wake, Waziri Mkuu amemhakikishia Bw. Bakhresa nia ya Serikali ya
Awamu ya Tano kushirikiana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda
kwani imedhamiria kukuza uchumi wa Tanzania kupitia uzalishaji wa
viwandani.
“Serikali
inathamini mchango wa wenye viwanda katika nchi yetu. Tunawashukuru
ninyi ambao ni wakongwe kwenye sekta hii, na kwa hiyo tunawaomba msikate
tamaa, muendelee kufungua viwanda zaidi ili wananchi wetu wapate mahali
pa kuuzia mazao au bidhaa zao,” amesema.
Amemuomba Bakhresa aangalie maeneo mengine zaidi ya kuwekeza kama vile sekta
za hoteli na utalii ili kusaidiana na Serikali kukuza uchumi wa
Tanzania.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI