WATAHINIWA 795,761 wanatarajia kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE)kwa siku mbili,kuanzia leo na kutaraji kumalizika kesho.
Mtihani huo unaofanyika nchini kote,ndio utakaoanza kutoa dira ya maisha kwa vijana hao,baada ya kupata elimu ya msingi kwa kipindi cha miaka saba .
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alisema wanafunzi 372,883 ambao ni sawa na asilimia 46.86 ni wavulana na wasichana ni 422,878 ambao ni asilimia 53.14.
Mwaka 2015 watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 775,729 huku 763,602 ndio waliofanya mtihani huo na wanafunzi 518,034 walifaulu.
Dk Msonde alisema watahiniwa 765,097 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 30,664 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa wakiitumia katika kujifunzia. Masomo yatakayotahiniwa ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na Maarifa.
Alisema watahiniwa wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 95 wakiwemo wavulana 57 na wasichana 38 wakati wale wenye uoni hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 810 ambao kati yao wavulana ni 402 na wasichana ni 408.

Amesema Maandalizi ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa
karatasi za mitihani, fomu maalum za kujibia mtihani na nyaraka zote
muhimu katika halmashauri na manispaa zote nchini,huku akitoa wito kwa kamati zinazosimamia kufanya kazi kwa weledi.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI