MFUNGWA katika gereza la
Wilaya ya Kahama,Shadrack William(32)ambaye ni mkazi wa Ushirombo mkoani Geita,anayetumikia
kifungo cha miaka 30 jela,kwa kosa la kulawiti amefikishwa tena Mahakamani kwa
tuhuma za kumlawiti Mahabusu wa gereza la mjini Kahama.
Akisoma shitaka hilo jipya
mbele ya Hakimu mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Kahama,Iman Batenzi,Mwendesha Mashitaka
wa Jeshi la Polisi,Felix Mbisse,alidai mfungwa huyo;Shadrack alitenda kosa hilo
septemba 10 mwaka huu.
Mbisse alisema Shadrack
anayetumikia kifungo kwa ajili ya kosa la kulawiti amerudia tena kosa hilo
gerezani humo, kinyume cha sheria nambari 154 (1) (a) ya makosa ya jinai
sura 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Aidha katika Mahakama hiyo
ilimpandisha kizimbani mkazi wa kijiji cha Mbika,Kata ya Ushetu,wilayani Kahama
ambaye ni mahabusu katika gereza hilo,kwa tuhuma za kukubali kulawitiwa na
Shadrack, ambapo ni kwenda kinyume cha sheria nambari 154 (1) (c) ya
makosa ya jinai shitaka ambalo pia amelikana.
Washitakiwa wote wawili
wamekana mashitaka dhidi yao hayo yaliyomo kwenye shauri la jinai nambari 547
la 2016 huku mahakama ikiliahirisha shauri hilo hadi Septemba 28,mwaka huu
litakapotajwa tena.