Kutokana
na wasichana hao wengiwao katika kipindi hicho kuwa na mahitaji
makubwa,ya kuingia katika maisha ya unyumba, wanapokosa uangalizi na ushauri
makini huwa chanzo cha kuharibu maisha yao.
Kwani
mara baada ya kupevuka kwao kunakoambatana na kutawaliwa na mhemko wa kuhitaji
ngono,pindi wakishindwa kujisimamia na kupata maelekezo mazuri ya walezi
wao,wanaume huwageuza dampo kwa kuhifadhi ashki zao pasipo kuwa na malengo ya
kufunga ndoa.
Ni
wazi wanaume hao Wakware,hutambua udhaifu huo wa wasichana ambao wanaona
kutekeleza tendo la akidi katika zama hizi ni kama mti wa tunda la Tufaha(Apple)
kumea jangwani,hivyo hutumia hamu hiyo kutongozea na kuwanasa kadri wanavyotaka
na kustarehe nao.
Vijana
wa Kiume sambamba na waume wakware wasio na staha,hutumia udhaifu huo kupata
warembo wa kustarehe nao pasipo kuhangaika kumwaga sera,kwani neno dogo tu,
“….mtoto mzuri nahitaji uwe mchumba wangu,”huwa pigo takatifu linalomaliza
akili ya wasichana wenye kiu ya kuolewa,na kuwapa uhuru wanaume wazinzi wa
kutenda watakalo.
Mtego huo wenye kauli hiyo, umeshindwa kuepukika
kwa wasichana pasipo kujali viwango vya elimu zao;umewaathiri
mashuleni,vyuoni,majumbani hata
makazini,kwani wasichana lukuki umewanasa
na kuwaingiza katika hesabu za Wakware hao,kuwa ni miongoni mwa
waliotumika mithili ya mua kwa kunyonywa maji yake kisha kapi lake kutupwa.
Hakuna
ubishi katika mzunguko wa dunia ya mapenzi,asilimia tisini na tano nukta tisa,walioitwa
wachumba, wamejikuta katika majuto, machungu na kilio.Wavulana waliowapa matumaini ya
kuwaingiza katika familia ya ndoa,waliwatema kisha kutekeleza tendo la akidi na
wasichana wengine.
Vijana
hao huwaacha solemba wenzi wao hao na kwenda kufunga pingu za maisha na
wasichana ambao kwa yakini, awali hawakuwa katika historia na fikra za Wanaume
hao kuwa ndio waliowataraji, kuwa nao katika safari yao ya unyumba ndani
ya maisha yao.
Je
madhila hayo yanayowakumba wasichana hao ya kuingia katika mitego ya hadaa,kuwa
wataolewa,kuna mwanamke yeyote,aliishaketi akatafakari na kubaini nini sababu
ya kutumika kama kapi la mua,ambalo mlaji hufyonza juisi yake kisha kulitupa?
Matamko
ya “My Sweet,My Nurse Love,My Wife,My Husband to be..”na mengine kibao,hukoma
ghafla kama mshumaa unaopulizwa na upepo,huku wasichana hao waliokuwa na
matumaini makubwa ya kuolewa wakiachwa na maumivu yasiyo mithilika,pasipo
kutambua kiini chake.
Ukitazama
makundi ya wasichana wa leo,utagundua kuwa wengi wao miongoni mwao wamejiweka
katika fungu la wanawake wa kustarehesha na si wa kuoa.
Saikolojia
inabainisha kuwa mavazi ya mtu apendayo kuvaa ndio utambulisho fika wa mwenendo
na tabia yake.Hivyo wasichana hao hujiweka katika mkondo wa dunia ya
kustarehesha wanaume kwa kielelezo hicho.
Ni
yakini kwamba mavazi ya mabinti hao yamejaa azma ya kutafuta ushawishi wa
kuwapata wanaume na abadani si kwa lengo halisi la kujistiri utupu kama lilivyo
kusudio la mavazi.Kutokuwa na mavazi yenye staha ukiongeza na tabia zao
zinazochagizwa na shauku ya ngono,wanajidhihirisha wazi kwa viwango
visivyowastahiki kuwa wanawake bora ndani ya familia.
Na
ifahamike kwamba,wanaume wengi wanavutiwa zaidi na tabia za wasichana wa
kustarehesha kuliko wale wa kuoa.Ni nadra sana msichana mwenye mavazi ya
heshima,kuwatoa macho wavulana walioketi kijiweni,tofauti na mwenye mavazi
yasiyo ya staha.
Zingatia
jambo moja,kinachowasukuma wavulana hao sio nia ya kuoa,bali kujipatia wakata
kiu ya mapenzi.Wao wanaamini kuwa katika dunia wanayoishi kuna wasichana
wanaostahiki kufunga nao ndoa pia wapo mahsusi kwa ajili ya kustarehesha
tu.Lakini hii imebaki ni siri ndani ya mioyo yao.
Kwa
kutambua kwao hivyo,licha ya ile mbinu ya kuongopea kuoa wanayotumia,pia huzidi
kuwapoteza wasichana kwa kuwatoa kwenye tabia njema hadi kuwa vyombo vya
burudani.Hiki ndicho kinachowaponza wasichana kuachwa na wapenzi wanaowataraji
kuwa waume zao wa kufa na kuzikana
Kimsingi
wavulana wa siku hizi,hususani hao wadanganyifu hawataki kuwa na wasichana
ambao wana aibu,wanahitaji vicheche wasiokuwa na soni ya kuingia nyumba za
kulala wageni nyakati zozote,ambao nguo za staha kwao ni adui nambari moja pia
wasioheshimu miongozo ya wazazi ama walezi wao bali husimamia matakwa yao.
Na
pindi wakiwapata wasichana ambao akili zao hushindwa kuzishikilia
wenyewe,huwashawishi kuvaa nguo fupi,zenye kuonesha maungo yao pasipo soni,ili
watoke nao hasa hasa usiku na kuwaingiza nyumba za kulala wageni pasipo
kusuasua.
Pia
huwatengeneza kutoogopa starehe ya aina yoyote huku wakiwa waongeaji sana wasio
na aibu kwa wanaume wa rika lolote,wanaojiona wako sahihi kwa kizazi hiki
kinachokwenda na wakati huku wakiweka asili na maadili yao kisogoni.Lakini
Ajabu pindi vijana hao wa kiume wanapohitaji kusogeza jiko la kufa na
kuzikana,huwakana wasichana hao waliowazoesha kuvaa nusu uchi na kwenda kuoa
wenye adabu zao na maadili mema ya Kibantu.
Ukiwahoji
kisa cha kutowaoa wapenzi wao wa awali watakujibu wale walikuwa wanastarehe nao
tu,kwani hawana staha na ni fedheha kuwaweka kuwa mama wa nyumbani,wenye
viwango vya kuoa si wao bali aliyemuoa ndio ana vigezo sahihi kuanzia maadili
na staha ya mavazi ndio maana kaamua kumuoa na kuachana na Changudoa.
Ni ajabu na inashangaza sana pamoja na madhila haya kuwakumba akina dada wengi,lakini bado hawajitambui,siku hadi siku makundi kwa makundi wamejikuta wakitumbukia katika kadhia hiyo.Hawashtuki kwa majuto yaliyowasibu waliowatangulia.
Huendelea kuwa vipofu kwa hofu ya kuwaudhi wawapendao,kwa
kujipa matumaini kuwa waliotendwa ilikuwa bahati mbaya na pengine
hawakupendwa,bali yeye ndio kapendwa naye kapenda,hivyo kauli ya mume ya kutaka
kukuoa tayari imehalalisha kuolewa kwake
na kukubali kila maelekezo ya kupotosha kutoka kwa wapenzi wao.
Anapokuwa
penzini hasikii la mzazi ama mlezi zaidi ya mchumba kibaka atakachosema, “…baby
leo vaa nguo ya kuonesha maungo yako tena ya kubana na fupi,kitovu kiwe nje na
mapaja hadharani kwani ndio mavazi yanayoenda na wakati.”Atatekeleza.
“Sweet
anza kunywa pombe maana unaniabisha kwa jamaa zangu kwa ukimya wako,lakini
ukinywa bia na kupata sigara utachangamka,pia hata tukiwa katika
malavidavi,hutakuwa na hiyana ya kunipa nitakavyo na kuniridhisha.”Atatenda,kinyume
na atakavyoambiwa na mzazi ama mlezi kuwa vitendo hivyo ni vibaya,atabisha.
Atatengenezwa
na mpenzi wake huyo wa kiume asiyekuwa na malengo ya kumuoa kiasi cha muonekeno
wake kuonekana ni fuska,nae kuyakubali matengenezo hayo,ambayo baadae huwa machungu
na majuto kwake baada ya kutoswa katika ndoa.
Mabinti
wa kileo hawatafakari na kujiuliza;Ni wasichana wangapi ambao awali walikuwa
wakilazimishwa na wavulana wao kwenda disko,kuvaa nguo fupi zisizo na staha ama
vichupi katika jamii iliyostaarabika,kujirusha viwanja usiku,lakini walipoolewa
walikatazwa kufanya hivyo?
Nini
kimewafanya wakatazwe?Maana kama kuna wanaume wapenda wanawake wa namna hiyo
kwanini wawakataze?Ni fika kwamba kuna wanawake wenye sifa za kustarehesha
wamebahatika kuolewa.Si ajabu hili kutokea.
Lakini
ni ukweli usiofichika wengi wao huingia katika hadaa ya wanaume wakware kwa
kutumika kama vyombo vya burudani,hawajali jamii inawatazama vipi na namna gani
wamejishushia heshima na kuzifanya familia yao zidharaulike?Hawana fikra wakati
huo kuwa wanapotezewa muda na kuharibiwa nao kuafiki jambo hilo,pindi wanapotelekezwa
ndipo hubaki wakigugumia kwa machungu.
Inashangaza
zaidi baada ya kukumbwa na madhila hayo badala ya kuketi chini na
kutafakari,hujikuta kwa kipindi kifupi wakiangukia katika mikono mingine isiyo
salama na hapo hubobea kuwa vyombo vya kuburudisha.
Ushauri
uliopo kwa watoto wa kike,ni vyema kama wangetulia.Abadani wasikubali kuingia
katika soko la kutafuta wanaume bila kujijua.Vivazi mvaavyo kwa madai ndio viendavyo
na wakati,vinawafanya mtamanishe na kuwa wanawake wa starehe,sio wa kuoa.
Kwani
vivazi hivyo vinawatega wavulana ambao hawapo katika mpango wa kuingia katika
mahusiano ya kufunga pingu za maisha kwa wakati huo,kuweni makini msiwakubalie
kwa kila wanalowaambia,wengi wao ni waongo hawana mpango mwema kwenu.
Jitahidini
kubadilika,mjithamini utu wenu na kutokubali kuingia katika mitego ya
kudhalilishwa.Mjiongoze katika maamuzi ambayo hayatakuwa na majuto hapo
baadae,kwa kuepuka vijana wa kiume wenye dhamira mbaya kwenu,wapimeni wanaume
wenye nia ya kufunga ndoa kwa kigezo cha kuwaongoza katika tabia njema.