MCHAMBUZI wa masuala ya siasa nchini,Julius Mtatiro amesema hana mpango wa
kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)licha ya kuwepo kwa fikra miongoni mwa wapenzi,mshabiki na baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaompa msukumo
mkubwa wa kumtaka agombee.
Hali kadhalika Mtatiro,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara),alisema haungi mkono Mwenyekiti aliyeyejiondoa katika wadhifa huo wakati wa chama hicho kikiwa katika Kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana,Profesa Ibrahim Lipumba,kurudi,kwa sababu siasa za Tanzania zinakokwenda zinahitaji viongozi wapya.

Katika
taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, Mtatiro ambaye pia ni mwanachama wa CUF,alisema kwa
kipindi kirefu amekuwa akipata msukumo kutoka kwa viongozi wa chama
hicho ngazi ya wilaya, wabunge, wafuasi na makada wa chama hicho kumtaka
ashiriki katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti.
“Katika
kipindi chote cha misukumo hiyo nimekuwa nikiwajibu wahusika wote kuwa
“sina nia ya kuchukua uongozi wa juu wa chama” kwa sababu bado nahitaji
muda wa kujiimarisha,” alisema Mtatiro katika taarifa yake.
Alisema
hata aliposhauri kuwa Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Profesa
Ibrahim Lipumba anapaswa kupumzika wapo walioona kuwa anatumia nafasi
hiyo kuutaka uenyekiti wa CUF jambo ambalo alisema si kweli.
Aidha,
Mtatiro alisisitiza kuwa hajawahi kuwa na nia ya kuutaka uenyekiti wa
CUF lakini hadi sasa msimamo wake ni kuwa haungi mkono Profesa Lipumba
kurudi katika nafasi yake kwa sababu siasa za sasa zinahitaji viongozi
wapya na wanaoweza kutazama mambo kisasa kwa mahitaji ya kizazi kipya.
Anasema; "....na wala sitachukua fomu kwa ajili hiyo,naomba tamko hili lifute misukumo,tetesi na kila aina ya taarifa kwamba ninayo nia au nitakuwa na nia hiyo."
Anasema; "....na wala sitachukua fomu kwa ajili hiyo,naomba tamko hili lifute misukumo,tetesi na kila aina ya taarifa kwamba ninayo nia au nitakuwa na nia hiyo."
“...
Na kwa sababu Profesa Lipumba anayo heshima kubwa kwa CUF na
watanzania, ni muhimu zaidi alinde heshima yake na abaki kuwa mshauri
mkuu wa chama. CUF ya sasa inahitaji mwenyekiti imara anayeweza
kukisimamia chama na kikajijenga lakini pia mwenye uwezo na ushawishi wa
kufanya siasa za ushirikiano na haki,” ilieleza taarifa hiyo.
Hata
hivyo, Mtatiro alisema anawatakia kila la heri wanachama wa CUF ili
waweze kuchagua mwenyekiti mzuri kwa ajili ya kukiendeleza chama hicho,
na kusisitiza kuwa jukumu lake litaendelea kukisaidia chama katika
masuala mbalimbali ya kiushauri.