MWITO umetolewa wa
kuharakisha ujenzi wa makao makuu ya
Halmashauri ya Msalala wilayani katika Kata ya Ntobo,sambamba na kuiomba
Serikali kufanya mchakato wa haraka wa kwa kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa
Isaka,ili kusogeza huduma zaidi kwa jamii.
Mwito huo ulitolewa na baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya wilaya ya Kahama,kilichoitishwa juzi na Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkulu,kubariki Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala kuhamishwa Busangi na kupelekwa Kata ya Ntobo.
Mjumbe kutoka Kata ya
Isaka,Gavana Ally,alishauri ni vyema Makao hayo yakajengwa haraka baada ya
kipindi cha mpito wa marumbano ambayo hayakuwa na tija zaidi ya kuchelewesha
maendeleo ya Halmashauri ya Msalala.
“…lakini kutokana na makao
makuu hayo kuwa mbali kiasi cha kuzifanya Kata zingine kuwa kisiwani,ni vyema
basi Serikali ikakamilisha mchakato wa kuanzisha Mamlaka ya mji mdogo wa
Isaka,ili kuzidi kusogeza huduma kwa jamii.”Alisema Gavana.
Katika Kikao hicho ambacho
Nkulu alikitumia kujitambulisha kwa wajumbe ambao ni wadau wa maendeleo
wilayani Kahama,wakiwemo na Madiwani wa Halmashauri ya Msalala,kilitumia dakika
27,kupitisha mapendekezo hayo ya kuhamishwa Makao hayo,kama alivyokuwa ameagiza
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,John Mongela.
Awali Mongela alipokuwa
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,alipitisha kwa maelekezo makao hayo yajengwe
Kata ya Ntobo,badala ya Mega,Segese na Busangi maeneo ambayo yaligubikwa na
mvutano wa kisiasa,hali iliyosababisha ujenzi wa makao hayo kukwama kuanzia
mwaka 2013,Halmashauri hiyo ilipoanzishwa.
Hata hivyo uamuzi wa
Mongela,haukufuata taratibu za upatikanaji wa Makao hayo,ikiwemo vikao vya
Kamati za Maendeleo ya Kata na kamati ya ushauri ya wilaya licha ya Halmashauri
hiyo,kuanza ujenzi kwenye Kata hiyo ya Ntobo.
Kufuatia hali hiyo
Nkulu,aliitisha kikao hicho akiwa na lengo la kutia Baraka kisheria ujenzi huo
uendelee,ingawa baadhi ya Wajumbe walipitisha uamuzi huo wa kujenga Ntobo kwa
madai wamechoshwa na mgogoro huo,kwakuwa wananchi wanahitaji maendeleo,pamoja
na eneo hilo kijiografia lipo pembezoni mwa Halmashauri hiyo.
Pamoja na Kikao hicho
kuwana agenda moja ya Makao Makuu hayo,Nkulu aliwaonya wadau wote kuzingatia
muda,uliopangwa wa vikao vyake.Kwakuwa yeye hataki watu wachelewe kwenye vikao
na kutumia muda mrefu kujadili agenda moja,alitaka wawe wanawahi kwenye vikao
na kutumia muda mfupi kujadili.
Kwa upande wake Albart
Wakati,mjumbe kutoka Kakola alimtaka Nkulu simu yake ya mkononi iwe wazi wakati
wote na akipigiwa awe anapokea haraka,hali ambayo Mkuu huyo wa wilaya alidai
atatekeleza hilo na kuwapongeza Madiwani wote na wajumbe wengine waliofika kwa
wingi kwenye mkutano huo.
Nae James Mhangwa mjumbe
kutoka Bugarama,aliwatahadhalisha wataalam wa ujenzi Katika Halmashauri
hiyo,kwamba katika eneo wanaojeng a Makao Makuu hayo,kuimarisha miundo mbinu
kutokana na hali halisi ya eneo hilo kujaa mafuriko ya maji wakati wa mvua za
masika.