WAFANYAKAZI
wa Mgodi wa Dhahabu Wa Acacia Bulyanhulu wamesherehekea siku ya
Mazingira Duniani kwa kufanya kazi ya kusafisha mazingira katika Kijiji
cha Ilogi kilichopo katika Halmashauri ya Msalala Wilaya
ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Akizungumza
wakati wa zoezi la usafi kijijini hapo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha
Ilogi Christopher Galila amesema hatua ya wafanyakazi kusafisha
mazingira ya kijiji ni funzo muhimu kwa wananchi wengine na kusema
kwamba uchafuzi wa mazingira hautavumiliwa katika maeneo yoyote
kijijini humo.
“Pamoja
na kutusaidia kusafisha hii leo meneo mbalimbali kwenye vizimba vya
uchafu ambavyo baadhi vimekuwa na taka kwa muda mrefu pamoja na soko
letu, Mgodi umetupatia mapipa kumi na tano ya kutupia taka ambayo
yatatusaidia katika siku za usafi za kila juma, kwani kijiji chetu kina
utaratibu wa kukusanya na kukagua usafi wa mazingira kila siku ya
Jumamosi.”
Naye
Kaimu Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Onesmo Kabeho
amesema timu ya wafanyakazi imefurahi mwitikio wa wananchi walioungana
na wafanyakazi kusafisha mitaa, mitaro, vizimba vya taka na soko
la kijiji.
“Sisi
leo tumefurahi sana kung’arisha maeneo mbalimbali kijijini hapa kwa
kuondoa kero ya uchafu ambao ni hatari kwa mazingira, tunatoa mwito kwa
wanajamii wote kutunza mazingira kwa njia mbalimbali ikiwemo
kudhibiti takataka hasa plastic ili watoto wetu na vizazi vijavyo
visipate athari ya uchafuzi wa mazingira wa sasa”.
Wafanyakazi wa Bulyanhulu Wakikusanya uchafu kwenye mitaro katika kijiji cha Ilogi.
Mfanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu Dennis Cowan akiwa amebeba Pipa la Taka wakati wa zoezi la kusafisha mitaa.
Usafi ukiendelea katika Mazingira ya Soko la asili katika kijiji cha Ilogi.
Wauzaji wa Mbogamboga wakifurahia zoezi la usafi Sokoni
Kaimu
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Onesmo Kabeho akikabidhi
mapipa 15 ya kutupia takataka kwa uongozi wa kijiji cha Ilogi.
Chanzo cha Habari ni Afisa Habari wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ;-Mary Lupamba.