GWIJI la Masumbwi Duniani,Mohammad Ali,amefariki dunia!
Bondia huyu wa
zamani ambaye alijiita ‘the greatest’,alikuwa ni miongoni mwa
watu maarufu na wenye wapenzi wengi duniani,amefariki
akiwa na umri wa mika 74 kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.
Bingwa
huyo wa dunia wa uzani wa juu wa zamani alilazwa hospitalini toka siku
ya alhamisi June 02 2016 kufuatia tatizo kwenye mapafu, Bondia huyo mbali na kupatwa na tatizo hilo alikuwa akiugua kiharusi.
Ali ambaye katika zama zake za masumbwi alikuwa na makonde mazito,huku akiwa mwepesi na mjanja anapokuwa ulingoni,alipatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984 baada ya kustaafu ngumi za kulipwa .
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI