MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu(BGML)unaomilikiwa
na Kampuni ya ACACIA,utaendelea kutoa fursa ya mafunzo kwa vitendo mgodini
hapo,kwa vijana wanaosoma elimu ya madini katika Chuo Kikuu cha Tanzania ili kuendeleza
sekta ya madini nchini.
Kauli hiyo imetolewa hivi
karibuni na Meneja Ufanisi na Uendelevu wa Mgodi huo,Elias Kasitila,alipokuwa
akikaribisha kundi la 42 la Wanachuo wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar
Es Salaam,wanaochukua mafunzo ya madini walioambatana na baadhi ya Wahadhiri
wao,ambapo alisema mgodi upo tayari kutoa kipaumbele ya mafunzo kwa vitendo kwa
vijana wanaochukua elimu hiyo kutoka Chuo Kikuu.
Kasitila alisema Kampuni ya Madini ya Acacia
imejipanga kuendeleza sekta ya madini nchini kwa kusaidizana na Serikali kwa
kutoa fursa kwa wasomi wanaosomea madini kufika kujifunza kwa vitendo hatua
itakayosaidia Taifa la Tanzania kupata Wataalamu wenye ujuzi stahiki wa madini.
"....kampuni yetu ina nia ya kusaidia sekta ya madini nchini,kwa kuchangia katika mchakato wa kuwaandaa kwa kuwapatia mafunzo ya vitendo wasomi tunaotarajia kuwa wahandisi wajao wa madini kupitia mpango,huu endelevu wa wanachuo kujipatia elimu kwa vitendo hapa mgodini."Alisema Kasitila.
Nae Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar Es Salaam,Geofrey William,alisema tangu makubaliano baina ya Mgodi na UDSM
kufanyika mwaka 2008,juu ya udhamini wa mafunzo kwa vitendo unaofanywa na
mwekezaji huyo,umesaidia kuleta ufanisi kwa vijana wanaochukua mafunzo ya
masuala ya madini.
Akitoa shukrani kwa mgodi uliotoa
fursa ya kuutembelea ili kujionea shughuli mbalimbali zifanyikazo
mgodini,Mhadhiri Dk.Richard Katemi,alivutiwa na utaratibu wa kiusalama
uliowekwa mgodini unaowawezesha watumishi,kwenda kazini na kurejea majumbani
salama.
Aidha alipongeza hatua ya Mgodi
kutoa fursa kwa wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam,wanaochukua mafunzo ya
masuala ya madini kupata mafunzo ya vitendo ambayo yamekuwa msaada mkubwa wa
kufahamu kwa kina walichokuwa wakijifunza chuoni.
“Ni kweli kwamba,sisi ni kawaida
yetu kuwafundisha wanachuo kwa nadharia,ziara kama hii husaidia kupata uelewa
zaidi,na zaidi husaidia kwa wanachuo kuziba pengo kwa kupata mafunzo kwa
vitendo,ambayo huwafanya kujifunza mengi yanayowaongezea tija katika
uwajibikaji wenye ufanisi wa shughuli za madini pindi wanapokuwa katika
ajira,”alisema Dk.Katemi.
Kwa upande wake Mwanachuo,Bahati
Moshally alisema ziara hiyo ya mafunzo,inasaidia kuongea ujuzi baada ya
kufanikiwa kupata mafunzo ya nadharia yanayokuwa muongozo wa kufanikisha
mafunzo ya vitendo,ambayo yanasaidia kufahamu zaidi masuala ya usalama migodini
mbali na utekelezaji wa uchimbaji unavyofanyika.
“Kwa tunayonufaika kwa
vitendo,shukrani zetu tunazitoa kwa uongozi wa Mgodi wa Acacia na Chuo Kikuu
chetu,kwa kujinga fursa hii adhimu kwetu wanachuo,”alisema Moshally.
Ziara hiyo ni ya nane kwa
wanachuo kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam,ambayo hufanyika mara moja kila
mwaka,na tayari zaidi ya wanachuo Elfu Moja wameishanufaika kwa kupata mafunzo
ya vitendo.
Chanzo cha Habari:Mary Lupamba.
| |||||||||||
KUNDI la Wanachuo wakiwa na wakufunzi wao wakianza ziara ya kutembelea mgodi kujionea shughuli za uchimbaji wa dhahabu. MENEJA wa Ufanisi na Uendelevu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Elias Kasitila akizungumza na Wanachuo wa UDSM,mara walipomaliza kutembelea chini ya ardhi kunakofanyika uchimbaji wa ardhi. |
MMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMAdd caption |
|