WAFUASI 22 wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) wakiongozwa
na Mratibu wa Chama hicho kanda ya Serengeti Renatus Pesa Nzemo wamefikishwa
Mahakamani.
Wanachama
na Wafuasi hao wa Chadema walikamatwa juzi na Jeshi la Polisi kwa
tuhuma za kufanya Mkusanyiko kinyume cha sheria wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi
wa Wilaya ya Kahama.
Waliofikishwa Mahakamani Renatus Pesa Nzemo{42}, Godwin Godson{34),
Amos Sipemba(41), Hamis Dominick (45), Rashid Ally(35), Emanuel Jidisha(48),
Method Marco(39), Athuman Martin(38), Ally Juma(29), Mashaka Masudi(23) na Cosmas
Thomas(26).
Wengine ni Simon Apolinary(24), Charles Elikana(27), Jovin Joel(20),
Enock Mosha(29), Zakayo Deogratius(44), Abeid Kapina(18), Omary Hassan(45), Kulwa Frank(28) , Yusuph
Ibrahim(38), Peter Jonas(41) pamoja na
Anthony Lauwo(35).
Wakisomewa Shitaka hilo na Mwendesha
Mashitaka wa Jeshi la Polisi Dismas Aniceth mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa
Wilaya ya Kahama Evodia Kyaruzi,
ilidaiwa kuwa Wahitakiwa hao walitenda kosa hilo 7/7/2016 majira ya saa 9.30
katika Uwanja wa CDT uliopo Mjini hapa.
Ilidaiwa kuwa kwa kufanya mkusanyiko kinyume na Sheria ya kifungu namba 74 na 75 ya
kanuni ya adhabu 16 kilichafanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Katika kesi hiyo namba 319 ya mwaka 2016 ilidawa kuwa watuhumiwa
hao walifanya mkusanyiko huo katika viwanja hivyo kwa lengo la kufanya uvunjifu
wa amani hali iliyosababisha jeshi la
Polisi kutumia nguvu kuwatawanya wanachama na wafuasi wa chama hicho
waliokusanyika kuwasikiliza viongozi wao.
Baada ya kusomewa Shitaka hilo Mahakamani hapo,Washitakiwa wote
walikana shitaka hilo na kufanya Mwendesha mashitaka kuomba tarehe kwa ajili ya
usiklizwaji wa awali kwa kuwa upelelezi wa Shauri hilo ulikuwa umekamilika.
Aidha Hakimu Kyaruzi aliwaambia Washitakiwa dhamana ipo wazi kwa
kila mmoja ambapo kila mshitakiwa
alitakiwa kuwa Mdhamini mmoja na dhamana ya shilingi 500,000 hata hivyo kesi
hiyo imeahirishwa hadi tarehe juni 16 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji wa
awali.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI