MWITO
umetolewa kwa Wananchi wa Tanzania,kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo
katika nchi za Afrika Mashariki,ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa
nchi, kutokana na kuwepo makubaliano,yaliyofikiwa na kuwapa wananchi wa nchi za
Afrika Mashariki kufanya biashara kwa uhuru.
Mbunge
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere,alitoa wito huo wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo,
jijini Dar es Salaam na kusema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinashirikiana kwa
mambo mbalimbali ikiwepo umoja wa forodha, soko la pamoja, umoja wa fedha na
shirikisho wa kisiasa.
Akiongea
na waandishi wa habari hao alitumia fursa hiyo kutoa wito huo kwa kubainisha
kupitia makubaliano hayo Watanzania wana nafasi ya kwenda kufanya biashara
katika nchi zingine bila kuzuiliwa na hivyo kuwa na nafasi ya kusambaza bishaa
zao katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alifafanua
kwamba ni wakati wa Wafanyabiashara wa Watanzania kuchangamkia nafasi zilizopo
za kufanya baishara kwa nchi za Afrika Mashariki, japo alikiri kuwa vikwazo
vilivyopo kwa sasa ni juu ya wananchi wengi wa Afrika Mashariki,hususani
Watanzania kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya jambo hilo.
Hata
hivyo alibainisha kwa upande wa Tanzania wamejipanga kuhakikisha fursa hizo za
kibiashara zinatumiwa vyema hasa baada ya kubaini changamoto hiyo ya wananchi
wengi kutokufahamu nafasi hiyo, wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa
Tanzania wataendesha programu ya kuwaelimisha Watanzania jinsi wanavyoweza
kunufaika na ushirikiano huo.
Alisema
programu hiyo ilianza Aprili 4 na itafanyika hadi Aprili, 23 ambapo kwa kuanza
wamepanga kukutana na Kamati za Bunge, Taasisi za Elimu ya Juu, vyombo vya
habari, kutembelea soko la Kariakoo na soko la Samaki la Feri.
Pia
Nyerere amewataka Watanzania kuwa na mazoea ya kutafuta taarifa mbalimbali
kupitia mitandao kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kukutana na fursa nyingi
ambazo hawakuwa wakizifahamu awali.