BAADHI ya wana hisa katika Benki ya CRDB,wanaomiliki hisa chache
Wilayani Kahama,wameiomba Benki hiyo kuwawezesha kuhudhuria vikao mbalimbali vya kitaifa
vinavyoandaliwa na taasisi hiyo,kwakuwa wana mchango katika kukua kwa taasisi
hiyo, badala ya wao kujitegemea kwa sasa.
Ombi hilo lilitolewa na Wanahisa hao wa Benki ya CRDB Tawi la
Kahama,katika kikao chao cha siku moja cha Wanahisa,ambapo mmoja wa Wanahisa
hao; Marco Nzela alisema kuwa wamekuwa wakishindwa kuhudhuria vikao vikuu
hivyo jambo linalosababisha kushindwa kuwasilisha changamoto zao na kusababisha
kupitwa na mambo mengi ya maana.
Alisema kuwa kama Benki hiyo ya CRDB ingekuwa inagharamikia wanahisa
wake katika vikao mbalimbali vinavyowahusu vya kitaifa kungekuwa na Wanahisa
wengi ambao wangekuwa wakihudhuria na hivyo kutoka na elimu zaidi
itakayowasaidia katika kukuza mitaji yao.
“Kwa sasa Wanahisa tunajigharamia wenyewe katika vikao hali ambayo
kwa sisi Wanahisa wenye hisa ndogo, inakuwa ni vigumu kuhudhuria kutokana na
kukosa fedha na hivyo kupelekea kutopata Elimu ya kutosha katika fani ya
biashara kwa ujumla”, Alisema Marco Nzela Mwanahisa wa Benki ya CRDB Kahama.
Aidha pamoja na mambo mengine Wanahisa hao waliuomba uongozi wa
Benki ya Benki ya CRDB Nchini kuhakikisha inabadili sehemu ya kufanyia mikutano
yake ya Wanahisa badaka ya kuweka katika Mkoa wa Arusha kila mwaka hali ambayo
inakuwa vigumu kwa wale wanaotoka katika mikoa ya pembezoni kuhudhuria.
Katika kikao hicho cha umma na Wanahisa wa Benki ya CRDB ambapo
kulitolewa mada mbalimbali kutoka kwa mtaalamu wa Benki ya CRDB ambaye pia ni
Mwanasheria Charles Lauwa Wanahisa hao pia walitakiwa kufungua akaunti ya
Busara ili kuweza kuongeza amana zao.
Lauwo alisema kuwa kati ya Wanahisa 11,500 waliolipwa gawio
kupitia Benki yaCRDB kwa mwaka 2014 kupitia akaunti za Benki, 11881
walilipwa klupitia katika akaunti ya Busara huku waliobaki wakilipwa kupitia
akaunti nyingine.
Aidha Mkufunzi alisema kuwa hata kama unakuwa na hisa katika
Makampuni mengine unaweza pia kutumia akaunti hiyo ya Busara
ambayo kwa ujumla inashirikisha watu wote na pia inamtambulisha mteja katika
neo husika aliloweka hisa zake.
Hata hivyo Lauwo alisema kuwa akaunti hiyo ya Busara
hufunguliwa kwa fedha za kitanzania na kuongeza kuwa amana
unazotakiwa kuweka katika akaunti hiyo ni kuanzia kiasi cha shilingi
200,000 huku kiasi cha riba yake ikiwa ni asilimia tatu kwa kwaka.
Hata hivyo Lauwo alisema kuwa ili kuweza kufungua akaunti ya
Busara lazima uweze kukidhi vigezo vyake kama vile vya kuwa miliki
wa hisa katika Kampuni iliyoorodheshwa katika sko la his alas Dar
es Salaam (DSE) na kuongeza kuwa pindi ukifungua akaunti hiyo amana yako
itaingia moja kwa moja.