RAIS wa Jamuhuri ya Sudani Kusini, Jenerali Salva Kiir akiwa pamoja na viongozi waandamizi katika serikali anayiongoza,ametia saini mkataba wa kujiunga na
Jumuiya ya Africa Mashariki(EAC) ikiwa ni hatua ya nyingine ya kuivusha nchi
yake na kuiongezea ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na maendeleo
ya watu wake.
Nchi ya Sudani Kusini inafikisha muunganiko wa nchi sita(6)hivi sasa baada ya Rwanda na Burundi kuwa miongoni mwa nchi hizo zinazounda jumuiya hiyo nyingine ni Tanzania ambayo hivi sasa Rais wake Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa EAC.pia zimo nchi za Uganda na Kenya.

Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya EAC ,Rais Magufuli amesema uchumi wa nchi hizi utakuwa kwa kasi kwani hivi sasa watakuwa na soko
kubwa la kibiashara na uzalishaji bidhaa.
Akitoa pongezi zake kwa wanachama wa EAC Rais Kiir
amesema atakuwa na ushirikiano wa kutosha na wanachama wenzake na
kudumisha Amani kwakuwa kwa kiwango kkikubwa utamaduni wa nchi hizo wanachama unashabahiana.
HABARI NA JACKSON BAHEMU.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI
HABARI NA JACKSON BAHEMU.