MKUU wa mkoa wa Mwanza,John
Mongella, ametoa wiki moja kwa uongozi
wa Jiji la Mwanza, kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika
eneo la Bugando,kwa mmiliki wake halali,Justine Eminoga, ambacho amekuwa
akikidai kwa kipindi cha miaka sita baada ya kupokwa na mfanyabiashara wa
Jijini humo.
Hatua hiyo ya Mkuu wa Mkoa
kutoa agizo hilo imefikia,mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa Justine
ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake hilo.
Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa
mkoa,Justine alidai kudhurumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara aliyemtaja kwa
jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba.
Katika hatua nyingine mkuu
huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha
wanakamilisha zoezi la kuhakiki watumishi, ili kubaini endapo kuna
watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo
linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati maalumu
zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo.
Akiwa katika ziara hiyo mkuu
huyo wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la Mwanza
Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua mikopo ya zaidi
ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata hivyo taarifa kutoka
Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani Mwanza iliyotolewa
wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani humo, ilisema mtuhumiwa huyo
tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi hiyo kwa mahojiano zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo
katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake ya tatu
mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI