Wednesday, April 13, 2016

MKOMBOZI WA SIASA NCHINI NI MABORESHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO





WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Sheria wamepewa rai ya kushikamana na Serikali katika kuhakikisha kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka1992 na Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 yanafanyika ili kuondoa utata na migongano ya utekelezaji wa masuala ya siasa nchini.

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja
Hayo yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akijibu swali kutoka kwa wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam ambao walihoji uhalisia wa utekelezaji wa sheria zililizopo sasa.

Kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
Wajumbe hao walihoji utitiri wa vyama vingi nchini ambavyo miaka nenda rudi havina madiwani wala wabunge na vingine kutoshiriki katika chaguzi . Wajumbe pia walihoji gharama ndogo za usajili wa vyama vya siasa ukilinganisha na hali ya maisha iliyopo kwa sasa.

B7
  Katibu kiongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria,Angelina Sanga,
Jambo lingine ambalo wajumbe wamehoji ni nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika kushughulikia migogoro ya kisiasa ndani na nje ya Vyama vya Siasa na ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi ndani ya vyama vya siasa.

Mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Richard Ndassa  akiwasilisha hoja
Akijibu hoja hizo Mhe Mhagama amesisitiza kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za uchaguzi ndio njia pekee itakayompa meno Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

 “Sheria tulizonayo ndio inatoa mwanya wa haya yote haya na ndio maana Serikali kwa sasa inaendelea na taratibu za kuboresha sheria hizi, tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ameshawasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Vyama vya Sasa na Sheria ya gharama za uchaguzi na sisi tumeridhia , tunasubiri tu bunge kujadili ili ziweze kutumika”alisisitiza mhe Mhagama.

CHANZO CHA HABARI NI KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI