Friday, April 15, 2016

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUKUZA UTAMADUNI WA AFRIKA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



MA1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akisaini makubaliano ya kuikaribisha Sudan kusini katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
RAIS wa Jamhuri ya Sudani ya Kusini Salva Kiiri  amesema uamuzi wa nchi yake kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki haujalenga kunaimarisha ujirani ulipo baina ya nchi hizo, bali unaimarisha ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki sambamba na raia wake ikiwa ni pamoja na kuendelea kukuza utamaduni wa Afrika.

Akitia saini makubaliano ya mkataba wa kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam,alishukuru Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,kukubali Sudani ya Kusini kuwa mwanachama wake.

Alisema kutokana na kukubalika kujiunga na Jumuiya hiyo,alifafanua kuwa sasa Sudani ya Kusini imepata sehemu sahihi kwa kujiunga na Jumuiya hii ambayo inalenga kuleta maendeleo kwa wananchi wake” amesema Rais Kiir.

MA3
RAIS wa Jamhuri ya Sudani ya Kusini Salva Kiiri
Rais Kiir amesema “tunajua malengo makubwa ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na kushuhudia kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mfano bora Afrika na duniani kwa ujumla.

Aliongeza kuwa Sudani ya Kusini imeona fursa zilizopo katika Jumuiya hii ikiwa ni pamoja na soko la pamoja (Common markert). Tayari tumetengeneza mifumo itakayosaidia ushiriki wetu katika Jumuiya ikiwemo kuanzishwa kwa Wizara itakayoshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mbalimbali zitakazowezesha kupatikana kwa Amani ya kudumu nchini humo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambaye pia ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amepongeza juhudi zilizofanywa na Sudani ya Kusini na hatimaye   kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ikiwa ni muda mfupi tu tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mnamo  Julai 20, 2012.

Rais Magufuli amesema kuwa siku zote Sudani ya Kusini imekuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa uchumi wake, utamaduni wake, lugha pamoja na historia yake na inaunganishwa na nchi za Jumiya hii kwa barabara pamoja na mto Nile.

Aidha, Rais Magufuli “alisema malengo ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji, kutoa bure huduma na uhuru wa wananchi kwenda popote ndani ya Jumuiya. 

Hata hivyo, Jumuiya hii inakumbwa na machafuko ya mara kwa mara na kuwa kikwazo kwa maendeleo ya uchumi wake”.
MA2
Add caption
Alisema Sudani ya Kusini imekubaliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kuwa imetimiza makubalino yaliyowekwa na Jumuiya ikiwemo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi, Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa Sudani ya Kusini inakuwa mwanachama wa sita wa Jumuiya hiyo, na kuwa ushirikiano wa kiuchumi uliopo katika nchi hizi utakuwa mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea.

Sudani ya Kusini iliomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki mnamo Novemba 10, 2012, ikiwa ni chini ya miezi minne tangu nchi hiyo ipate uhuru wake.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI