Friday, April 15, 2016

DIAMOND KUFANYA MATAMASHA BARA LA AFRIKA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

DIAMOND na mama yake nchini Marekani.
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva nchini,Nasibu Abdul " Diamond"ambaye hivi karibuni amefanya "show" barani Amerika akiambatana na familia yake,amedai yupo katika maandalizi ya kutoa burudani katika bara la Afrika,pindi atakapokamilisha kutoa nyimbo maalumu kwa ajili ya Bara la Afrika.

Diamond ambaye katika matamasha yake nchini Marekani yalikuwa ya mafanikio makubwa  kutokana na kukubalika kiasi cha matamasha yake kuhudhuriwa na watu wengi ambayo aliyafanya katika Arena zinazotumiwa na wasanii wakubwa wa nchi hiyo,huku baadhi ya wasanii wengine wakishindwa kufikia mafanikio ya kujaza umati wa mashabiki kama ilivyotokea katika matamasha yake.

Msanii huyu mwenye jina kubwa barani Afrika amesema ameona kuwa mziki wa bongo fleva umekuwa mkubwa sana duniani kwani alijaza kumbi ambazo hata baadhi ya wanamuziki wa Marekani wakifika wanafanyia kule kwa sababu sio kila msanii wa marekani anaweza kujaza Arena hizo.

Ametanabaisha baada ya matamasha hayo kuwa na mafanikio,sasa yupo mbioni kufanya matamasha hayo katika bara la Afrika pindi atakapokamilisha tungo zenye nyimbo mahsusi kwa ajili ya wapenzi na mashabiki wa muziki huo kwa bara la Afrika kuwa zimetoka.


Aidha  Msanii huyo amesema hii ni mara yake ya kwanza kusafiri na familia yake, kama mama yake hajawahi kwenda ulaya kabisa hivyo ameamua kumtoa ushamba.
"Miaka inaenda na tangia 'nimetoboa' sikuwahi kusafiri na mama yangu kwanza hakuwahi kwenda Europe au Ulaya alikuwa anaisikia tu kwenye bomba, inaweza kuwa kesho au kesho kutwa nikadondoka nikafa halafu mama yangu akabaki tena kuisikia nikaona ni bora kwenda kutoana ushamba kabisa"

Aidha msanii huyo amesema ataendelea na 'tour' yake ambapo atafanya 'show' 3 marekani, na pia 'show' nyingine zitafanyika India, Dar es Salaam , Mwanza, na Australia.

 

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI