HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo “CHADEMA” na familia ya Mwenyekiti wa CHADEMA Geita Alphonce Mawazo wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi lililozuia mwenyekiti huyo,asiagwe jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga.
Taarifa kutoka Mahakama kuu
Kanda ya Mwanza zinaarifu
kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameruhusiwa kuendelea
na taratibu za kuaga mwili wa marehemu na kuzika, huku Polisi wakitakiwa kutoa
ulinzi kama ilivyo wajibu wao kwa kuzingatia mipaka ya kazi yao.Akitoa hukumu hiyo,Jaji Lameck Mlacha,alisema Mahakama Kuu Jijini Mwanza imetoa ruhusa mwili wa Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na kisha kuuzika mwili wa mpendwa wao huyo ila wafuate tu utaratibu,huku ukiliagiza Jeshi la Polisi kutoa Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.
Kulikuwepo sintofahamu
juu ya hatma ya kuuzika mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Geita Mawazo
baada ya kutokea kwa mvutano kati ya UKAWA na Jeshi la Polisi.
Ambapo Jeshi la polisi lilitoa amri kuwa
Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu,huku familia kwa
kushirikiana na UKAWA ikipinga amri hiyo,ambayo imetupiliwa mbali na Mahakama
hiyo.
Katika kesi hiyo Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe walikuwa wakiongoza wafuasi wa UKAWA waliokuwa wakihudhuria mwenendo wa kesi hiyo,ambapo upande wa Mashitaka uliongozwa na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallya.