JUMLA
ya Shilingi Milioni 36 zinatarajia kukamilisha vyumba vitatu vya maabara na
ofisi tatu katika shule ya sekondari Bugisha iliyopo Kata ya Mondo wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.
Hayo
yalisemwa na Diwani wa Kata ya Bugisha Said Hamad, wakati akiongea na Gazeti
tando hili katika shule hiyo ambapo ujenzi huo unaendelea.
Alisema
maabara hiyo inajengwa kwa nguvu za wananchi na itakapofika mwezi Desemba mwaka
huu ujenzi wa maabara hizo utakuwa umekamilika kadri ya maagizo ya
serikali.
Hamadi
aliwaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano ili kukamilisha
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wa shule
zote za kata kuwa na maabara.
Aidha
Said aliipongeza Halmashauri ya Mji kwa kutoa tofali 4,000 kwa kila Kata ili
kuweza kukamilisha ujenzi huo ambapo mchango huo umeongeza nguvu zaidi
kwa wananchi na kuendelea kuwa na imani na serikali iliyopo madarakani.