MSHAMBULIAJI Elius Maguli wa Simba akiwatoka mabeki wa Yanga. |
WATANI wa jadi na timu kongwe nchini Yanga na Simba zimetoshana nguvu katika pambano kali la Ligi kuu Tanzania Bara,lililochezwa uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.
MASHABIKI wa Yanga wakifuatilia pambano |
Katika
pambano hilo ambalo macho ya washabiki yalikuwa kwa washambuliaji Denilson Jaja
wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba kuwa watazisaidia nini timu zao,lilimalizika
pasipo kufungana huku kipa wa Simba Peter Manyika akionyesha umahiri mkubwa
katika kulinda lango.
HOFU;Ilikuwa kosakosa langoni mwao |
Manyika
ambaye Yanga walidai akiketi langoni watammiminia mvua ya magoli,alionyesha
utulivu wa hali ya juu na kuisaidia timu yake isipachikwe bao.
Kinda huyo alianza kuonyesha umahiri wake wa
kulinda lango mnamo Dakika ya 13,baada ya Jaja kutuliza mpira katikati ya mabeki ya
Simba kisha kuachia shuti kiufundi, lakini Manyika alilidaka shuti hilo kwa
umaridadi mkubwa.
AKINA Dada hawa ni mashabiki kindakindaki wa Yanga |
Mnamo Dakika ya 17 Okwi alitengenezewa mpira mzuri na Shabalala lakini shuti kali lilitoka nje kidogo.Na Yanga walijibu shambulizi hilo sekunde 36 baadaye,lakini Manyika JR anafanya kazi kubwa kwa kutoka na kulidaka shuti la Coutinho.
Dakika
ya 18, Okwi aliyeonekana mwiba kwa mabeki wa Yanga alituliza mpira kifuani na
kumzidi maarifa Juma Abdul,akiwa mbele ya Cannavaro,alimhadaa na kuachia kombora
lililotoka juu kidogo ya lango la Yanga.
MASHABIKI wa Yanga wakiilaki timu yao |
Mnamo Dakika ya 72,Manyika
alifanya kazi ya ziada tena baada ya kutoka na kuuwahi mpira aliokuwa nao
Mrisho Ngassa aliyefaulu kuingia eneo la hatari baada ya kupokea pasi safi ya
Coutinho.
Kipa kinda huyo wa Simba
alizidi kudhihirisha umahiri wake mnamo Dakika ya 77,baada ya kuokoa shuti la
Coutinho aliyekuwa peke yake akimtazama.
Mshambuliaji wa Simba
Haruna Chanongo mnamo Dakika ya 84, alifanikiwa kuisambaraisha ngome ya Yanga
lakini shuti lake kali lilipaa juu ya lango la Yanga.
MNAZI wa Simba wa Jacob Steven "JB" na Shabiki wa Yanga Irene Uwoya wakifanyiana ufyosi kabla ya pambano. |
Katika pambano hilo Yanga
waliokuwa mwenyeji wa mchezo huo,walipata kona nne na Simba kona tatu.
HUKO Mtwara, Ndanda
FC imeonja utamu wa kufungwa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 3-1 na JKT Ruvu.
Ndanda imefungwa mabao hayo ikiwa
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mabao ya JKT Ruvu yalifungwa na Juma
Ndeule, Abrahman Mussa na Thomas Matayo.
Mjini
Morogoro, Polisi Moro na Mtibwa Sugar zimemaliza dakika 90 bila ya kufungana.
Nako Jijini Mbeya bao la nahodha Aggrey
Morris ndiyo ‘sumu’ iliyoimaliza Mbeya City huku Azam FC ikiibuka na ushindi wa
bao 1-0.Na kuifanya Mbeya City kuendelea kuwa wateja wa wana lambamba.
Licha ya kuwa nyumbani, Mbeya City ilishindwa
kuizuia Azam FC baada ya bao hilo moja la Morris lililofungwa kwa mkwaju wa
adhabu baada ya Kipre Tchetche kuangushwa nje ya 18.
Mara ya mwisho zimekutaka kwenye uwanja
huo ilikuwa ni mechi ya kufunga msimu na Azam FC ikashinda na kubeba ubingwa.
Mjini Tanga, Coastal Union imeshinda
kwa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo.