![]() |
DCP Mohammed Mpinga |
JESHI
la polisi nchini limewaonya askari wa kitengo cha usalama barabarani kuacha
vitendo vya kupokea rushwa ili kuzuia ajali za barabarani zinazoendelea
kupoteza uhai wa watu wasio na hatia huku zikiwaachia wengine ulemavu wa
maaisha.
Kauli
hiyo ilitolewa mjini Dodoma na Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,DCP Mohammed Mpinga
alipowahutubia wakurugenzi na mameneja wa Radio Jamii nchini kwenye mkutano wa
siku nne na wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao kimawasiliano.
Mpinga
alisema, jumla ya watu 4,000 wanapoteza maisha kila mwaka kwa ajali za
barabarani ambazo Chanzo chake kikubwa ni makosa ya kibinadamu kama uzembe wa
madereva, ulevi, mwendo kasi, kutozingatia sheria na uchovu wa safari.
Aliendelea
kusema kuwa sababu nyingine ni matumizi ya vyombo vya moto pasipo kupata
mafunzo, huku ukaguzi na usimamizi unaofanywa na askari wa usalama barabarani
ukugubikwa na wimbi la rushwa.
Mpinga
aliziomba radio za jamii kushiriki kwa kina katika kuwaelimisha wananchi kwamba
wanayo nafasi kubwa ndani ya jamii kukomesha ajali hizo kwa kuhakikisha
makondakta hawashiriki kutoa rushwa kwa askari wakati wanapokuwa wamekamatwa na
makosa.
Alisema
jeshi la polisi limekwishatoa maelekezo
dhidi ya askari kumchukua kondakta pembeni na kumtoza rushwa hali ambayo ni
sawa na kuuza maisha ya abiria wanaosafiri na gari husika.
Mpinga
alisisitiza kuwa adhabu anayotozwa kondakta inatakiwa iandikwe mbele ya abiria
na wala siyo kweye gari la askali, kivuli wanachokuwa wanapumzika wakiwa
kazini, na wala siyo kuwekwa kwenye nyaraka za gari mithili ya kwamba
zinakaguliwa.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa mtandao wa radio jamii nchini COMNETA, Joseph Sekiku
alimthibitishia Mpinga kwamba, radio hizo zinazowafikia zaidi ya wasikilizaji
milioni 16 nchini, zimekubali kushirikiana na ofisi yake katika kutoa elimu ya
usalama barabarani.
Nao
Wajumbe 48 waliohudhuria kikao hicho wamemwomba mpinga kutoa ushirikano wa kina
pale ofisi yake inapohitajika na kuchukua hatua mwafaka kwa matukio
yatakayotolewa kwa vielelezo makini dhidi ya watu wanaorudisha nyuma juhudi
hizo.