![]() |
SACP Liberatus Sabas |
JESHI la Polisi mkoa
wa Arusha limefanikiwa kumuua kwa kumpiga risasi Yahaya Hassani Omary
anayetuhumiwa kuwa ndiye Kinara wa matukio ya
ulipuaji wa mabomu na
umwagiaji tindikali viongozi wa dini.Kamanda wa Polisi mkoani Arusha,SACP Liberatus Sabas Alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa tano na nusu katika barabara ya Babati mkoani Arusha wakati mtuhumiwa akijaribu kuwakimbia polisi.
Alisema mtuhumiwa huyo wa ugaidi mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu alikamatwa na kushikiliwa wiki mbili zilizopita mkoani Morogoro na aliuawa wakati akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.
Kamanda Sabas alisema Mtuhumiwa huyo alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani Morogoro lilimkamata,na baada ya kufanyiwa mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko Kondoa.
“Wakati
akipelekwa kuonyesha alipoyahifadhi,ndipo alipotumia mbinu zake ambazo
amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndipo
akapigwa risasi mbili"alisema Sabas.
Aidha
Kamanda Sabas alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu ili
kuweza kuteketeza matukio ya uhalifu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI