MWITO umetolewa kwa jamii kuona umuhimu wa kuwekeza elimu kwa mtoto wa kike huku wakihakikisha wanampatia mazingira mazuri yatakayomwepusha na mimba za utotoni
Hayo yalielezwa na Mbunge wa Jimbo la Msalala,Ezekiel Maige,katika mahafari ya 12 ya Shule ya Sekondari ya Mwalimu Nyerere,iliyopo Kata ya Segese,Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama,ambapo aliitaka jamii kuwekeza katika elimu pasipo kumbagua mtoto wa kike.
Aliasa jamii ya ukanda wa magharibi kuondokana na mila za zamani za kumnyanyapaa mtoto wa kike katika suala la elimu kwa kutoa kipaumbele pekee kwa mtoto wa kiume pasipo kutambua kila mtoto ana haki ya kupata elimu pasipo kujali ni wa jinsi gani.
Alisema
mtoto wa kike ana haki ya kupata elimu kama ilivyo kwa mtoto wa kiume na
kuwataka kuhakikisha wanamjengea mazingira mazuri ya kufanya vyema katika
mitihani yake ya mwisho kwa kwa kumuweka hosteli huku wakimlinda na kumpatia
maadili mema kwa maslahi ya Taifa.
“Niwaombe sana wazazi,tuwajengee mazingira mazuri watoto wa kike kuepukana na vishawishi kwa kuhakikisha mnafumbia macho gharama kwa kuwaweka hosteli ambako watapata fursa nzuri ya kushirikiana na wenzake katika kukuza taaluma.”Alisema Maige.
Awali wakisoma risala yao Wahitimu ,walieleza changamoto kubwa inayomkabili mtoto wa kike anaesoma ilhali akiishi nyumbani ni vishawishi kutoka kwa wanaume ambavyo vimekuwa adui katika kutimiza ndoto zao.
Walisema mazingira hayo yamesababisha kwa kiwango kikubwa wasichana wengi kupata mimba zizisotarajiwa wakiwa katika umri mdogo na kukatisha masomo yao huku wahusika waliosababisha kukatisha masomo kwa wasichana hao wakishindwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Tunaomba
wasichana tulindwe,pia vyombo vya sheria viwachukulie hatua kali wanaume
watakaobainika kuwakatisha masomo wasichana kwa kuwapa mimba,”Ilisema risala
hiyo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI