Saturday, September 13, 2014

JAMII ISIZIBEZE SEKONDARI ZA KATA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MIONGONI mwa wanafunzi waliofaulu katika shule ya Sekondari  Mwendakulima,wilayani Kahama;Veronica Samsoni [20] akipongezwa baada ya kutunukiwa cheti na Mkuu wa kitengo cha Sheria  kutoka Kampuni ya African Barrick Gold mine na Mkurugenzi wa Bodi ya Ufadhili ya Can Educate; Katrina White katika hafla ya kuwapongeza 15 waliofaulu vyema katika mtihani wao wa mwisho kuhitimu kidato cha sita kwa kupata Daraja la kwanza.
JAMII imetakiwa kuacha mara moja tabia ya kuzibeza Shule za Sekondari za Kata kwakuwa idadi kubwa yake zinaendelea kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali ya Kitaifa.
Changamotohiyo ilitolewa leo na Mkuu wa Shule ya sekondari ya Mwendakulima wilayani Kahama;Diana Kuboja wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi 15 kati ya 23 waliofaulu kidato cha sita kwa alama daraja la Kwanza katika shule hiyo.

NI mwanafunzi Theleza Maziku [20] akipewa cheti cha kupongezwa na Mkuu wa kitengo cha Sheria cha Kampuni ya African Barrick Gold mine na mkurugenzi wa Bodi ya Ufadhili wa Can Educate;Katrina White katika hafla ya kuwapongeza 15 waliofaulu kwa kupata Daraja la kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kata hiyo .
Katika hafla hiyo iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine kupitia mgodi wake wa Buzwagi,Kuboja alisema katika matokeo ya mwaka huu Shule yake ya Kata ya Mwendakulima wanafunzi wote  waliofaulu wamekwenda vyuo vikuu.

MMOJA wa wanafunzi waliofaulu katika shule ya Kidato cha Sita ya Sekondari ya Kata ya Mwendakulima Mary Joseph[19] akipewa cheti cha kupongezwa na Mkuu wa kitengo cha Sheria cha Kampuni ya African Barrick Gold Mine na Mkurugenzi wa Bodi ya Ufadhili wa Can Educate;Katrina White katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi 15 waliofaulu kwa kupata Daraja la kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kata hiyo 
Alisema Shule yake ni ya kwanza kimkoa na Kikanda ambapo kitaifa katika shule za wanafunzi wachache  180 imekuwa ya tisa,hali ambayo jamii inapaswa kuheshimu matokeo hayo,hasa kwakuwa darasa zima limefanya vizuri.
MWANAFUNZI Rachel Mtwale [20]akikabidhiwa cheti cha kupongezwa na Mkuu wa kitengo cha Sheria kutoka Kampuni ya African Barrick Gold Mine na Mkurugenzi wa Bodi ya Ufadhili wa Can Educate ya jiji la London Uingereza;Katrina White katika hafla ya kuwapongeza 15 waliofaulu kwa kupata Daraja la kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kata ya Mwendakulima.
Aidha aliiomba jamii pia iheshimu  ufadhili unaotolewa na kampuni ya Barrick kwa baadhi ya Wanafunzi,sambamba na kuchangia huduma mbalimbali za kijamii hasa katika sekta ya elimu jambo lililoleta hamasa ya wanafunzi wa sekondari hiyo kufanya vizuri.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi Dorothy Bikurakule akionyesha maajabu ya glasi yenye thamani ya Shilingi Elfu Ishirini kila mmoja ambayo walipewa zawadi walimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Mwendakulima katika hafla ya kuwapongeza,nyuma yake wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Diana Kuboja akifuatiwa na Meneja Mkuu wa Mgodi huo Philbert Rweyemamu,akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa kampuni ya Barrick Katrina White,glasi hiyo ikiwekewa maji ina uwezo wa kubadili rangi .
Naye Mkuu wa  kitengo cha sheria     cha Kampuni hiyo ya Barrick na Mkurugenzi wa Bodi ya Ufadhili wa Can Educate kutoka London Uingereza;Katrina White alisema Kampuni yake imeongeza Dola Elfu Tano kwenye ufadhili katika huduma za jamii katika maeneo iliko migodi yake ikiwemo wilaya ya Kahama.
MKUU wa kitengo cha Sheria kutoka Kampuni ya African Barrick Gold Mine na Mkurugenzi wa Bodi ya Ufadhili wa Can Educate;Katrina White akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi 15 wa shule ya sekondari ya Kata ya Mwendakulima,wilayani Kahama waliofaulu kwa kupata Daraja la kwanza kwenye mtihani wa kidato cha sita .

Kwa upande wake Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu aliitaka jamii kuwa mstari wa mbele katika suala zima la maendeleo kuliko kutegemea mgodi ambapo utasaidia pale wananchi walipoanzisha miradi yao wenyewe.


KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI