bNa Ali Lityawi
Kahama
Agosti 31,2010
WATIMULIWA KAZI MGODINI BUZWAGI KWA KUISHABIKIA CHADEMA.
• Maige na Mkuu wa Wilaya wadaiwa kuhusika na kutimuliwa kwa watumishi hao.
WAKAZI wawili wilayani Kahama wamejikuta wakikumbwa na adh ya kisiasa,kutokana na kutimuliwa kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi,unaomilikiwa na African Tanzania Barrick Mines kwa kuhusishwa na kukiunga mkono na kukishabikia chama cha CHADEMA.
Wakazi hao;Michael Jagi na Godfrey Makanda waliokuwa wakifanya kazi kampuni ya Pangea iliyo chini ya Mgodi wa Buzwagi Barrick,walifukuzwa kazi baada ya gari za mgodi walizokuwa wakizitumia kuziegesha eneo la Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kahama ambapo zipo Ofisi za Tume ya Uchaguzi wa Majimboya Msalala na Kahama,huku baadhi ya wafuasi na viongozi wa CHADEMA wakionekana karibu na magari hayo.
Akiongea na Tanzania Daima Jumatano,mmoja wa waathirika hao;Godfrey Makanda aliwatupia shutuma ,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Msalala;Ezekiel Maige pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kahama;Meja Mstaafu Bahati Matala kuwa ndio kichocheo kikubwa na walioushinikiza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi uwatimue kazi ,kwa kupeleka fitina kuwa wanatumia gari za Kampuni kusaidia harakati za CHADEMA kusaka Ubunge katika Jimbo la Msalala.
Makanda alisema kilichomponza siku hiyo ambayo ilikuwa ni siku ya mwisho ya kurejesaha fomu kwa wagombea,ni kuegesha gari katika eneo la Ofisi za Tume ambazo zipo karibu na Mahakama ya Mwanzo pia Mahakama ya Wilaya ya Kahama ambako alikuwa na shughuli zake binafsi,na aliporejea alikuta wanasiasa wa vyama mbalimbali akiwemo Naibu waziri;Maige wakiwa wamezizunguka gari hizo.
“ Nililazimika kuwasalimia wote waliokuwa karibu na gari yangu na ile ya Michael Jagi aliyekuwa Engineer Construction wa Pangea kabla ya kuingia kwenye gari na kuondoka,ndipo alipofika dreva wa Maige na kuanza kutuchukua picha ambazo nilidhani ni za kumbukumbu ya kawaida,kumbe walizipeleka kwa DC aliyepiga simu mgodini hatimaye tukatimuliwa kazi,’’ Alisema Makanda.
Alipohojiwa kwa njia ya simu na gazeti hili,mgombea Ubunge Jimbo la Msalala kwa tiketi ya CCM,Ezekiel Maige ambaye anachuana vikali katika nafsi hiyo na mgombea wa CHADEMA,Edward Mlolwa aliewahi kufanya kazi mgodi wa Barrick akiwa Meneja Ugavi,alikana kuhusika kufukuzwa kazi kwa watu hao kwa kuwa suala hilo ni lao na mwajiri wao.
“ Mimi siku – note hilo jambo,bali viongozi wangu wa Chama,ukweli lile gari moja lilikuwa likitumiwa na wenzetu,kwa macho yetu tukiona wakiingia na kushuka,Mwandishi wewew waulize kama Katibu wa CHADEMA;Muhidini hakupanda ile gari,sisi tukaona tuulize..,sasa hayo mengine ni yao na mwajiri wao iwapo walihojiwa wakashindwa kujitetea halituhusu,”Alisema Maige.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Meja Mstafu Matala awali alikana kutolifahamu suala hilo lakini baada ya saaa moja alipiga simu na kueleza kuwa anachofahamu ni kuhusiana na Michael Jagi kuingizwa katika matatizo yasiyomhusu na anafanya jitihada za kumnusuru arejeshwe kazini,lakini huyo mwingine kama alijihusisha ni budi aadhibiwe lakini yupo tayari kupokea malalamiko yake akiyawasilisha ofisini kwake.
Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA wa wilaya ya Kahama,Muhidini Mfwangavo alidai watu hao wameonewa bure kwani siku hiyo kila mtu aliyekuwepo eneo la tume wakiwemo wana CCM,na vyama vingine vya siasa waliitumia gari hiyo kujihifadhi kwa jua baada ya kuegeshwa eneo hilo na halikutumika kwa namna nyingine.
MWISHO
Tuesday, August 31, 2010
WAPOTEZA KAZI MGODI WA BUZWAGI KWA KUISHABIKIA CHADEMA
BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO