HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI

BUZWAGI WATAKIWA KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI VYA MICHEZO.
TIMU ya Waendesha baiskeli kibiashara "Daladala United wakiwa wenye shauku wakisubiri kusalimiana na Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Bonanza la soka lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine Ltd.

TIMU ya Wauza mbao wakisubiri kusalimiana na Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Bonanza la soka lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine Ltd.

AFISA Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi Dorothy Bikurakule akiongea katika Uzinduzi wa Bonanza la Soka,linalofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

MENEJA wa Mahusiano wa Mgodi Buzwagi akitoa neno kabla ya Uzinduzi wa Bonanza hilo "Daladala United " lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine Ltd.

AFISA Michezo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama;Julius Kambarage akiongea kabla ya Uzinduzi wa  Bonanza la soka lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine Ltd.

MGENI rasmi katika Uzinduzi wa Bonanza,Amani Sabasaba akiongea na wanamichezo mbalimbali sambamba na wadau wa michezo wakati wa uzinduzi wa Bonanza.
AFISA Elimu Taaluma kwa Shule za Msingi katika Halmashauri ya Mji Amani Sabasaba akikabidhi seti yajezi kwa Kiongozi wa Timu ya Afya FC;Hemedi Said Saady kabla ya kufanyika uzinduzi wa Bonanza.

TIMU za Daladala United wenye jezi nyeusi na Timber FC wenye jezi nyekundu wakisubiri uzinduzi wa Bonanza.

MGENI rasmi katika Uzinduzi wa Bonanza,Amani Sabasaba akisalimiana na wachezaji wa Daladala United.

MGENI rasmi katika Uzinduzi wa Bonanza,Amani Sabasaba akisalimiana na wachezaji wa Timber FC.

MENEJA Mahusiano wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi akisalimiana na wachezaji wa Timber FC

WACHEZAJI wa Daladala  United wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi na wa Halmashauri ya Mji
MWANDISHI wa habari akiwa kazini

MCHEZAJI wa Daladala United Feruzi Kabuye akimchambua kwa umaridadi kipa wa Timber FC Charles Maganga,na kuipatia timu yake bao la ushindi. 




HALMASHAURI ya Mji wa Kahama umeomba
 Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold Mine Ltd kuanzisha michuano ya michezo mbalimbali kila mwaka itakayosaidia kuibua na kuendeleza vipaji ambavyo vitasaidia kupunguza ombwe la ajira nchini.

Mwito huo ulitolewa na Afisa Michezo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama Julius Kambarage wakati wa uzinduzi wa Bonaza la Soka lililoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi linaloshirikisha makundi ya jamii yanayojishughulisha na shughuli mbalimbali za Kijasiriamali,ikiwemo waendesha baiskeli kibiashara “Daladala”,Pikipiki kibiashara “Bodaboda”Bajaji,Wakata tiketi za abiria pamoja na wauza mbao.


Kambarage alisema
 katika kuibua na kuendeleza michezo kwa vijana ni budi Mgodi ukaanzisha Kombe la Mahusiano ambalo litashirikisha kila kada ya michezo hatua itakayosaidia kuimarisha mahusiano sambamba na kusaidia ongezeko la ajira kwa vijana,hasa kwakuwa michezo hasa soka katika karne ya leo ni ajira.

Akifungua Bonanza hilo,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Amani Sabasaba aliwaasa vijana kutumia fursa ya michuano mbalimbali inayoandaliwa wilayani Kahama,kuimarisha vipaji vyao sambamba na kuzingatia maadili ya michezo ili waweze kufanikiwa kujipatia ajira kupitia sekta ya michezo.


Nae Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi Bahati Mwambene kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Mgodi;Filbert Rweyemamu alisema Bonanza hilo mbali ya kushirikisha timu za vijana kutoka makundi ya ujasiriamali lakini ndio itakayotumika kuteua wachezaji watakaounda timu ya Kahama Buzwagi itakayoshiriki michuano itakayo shirikisha Migodi yote ya Barrick.


Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Buzwagi Dorothy Bikurakule alisema Bonanza hilo limeshirikisha makundi mbalimbali ya ujasiriamali kama waendesha baiskeli kibiashara{Daladala}Bodaboda za pikipiki,wauza mbao,wasanii wa maigizo na watumishi wa serikali ili kuwaweka pamoja katika kujenga mahusiano mema baina yao na Mgodi.


Bonanza hilo linaloshirikisha timu nane ambazo ni Timber FC,Daladala United,Wasanii FC,Stendi Sport Club,Bajaji FC,Bodaboda FC,Halmashauri Sport Club na Afya FC linatimua vumbi kwa mtindo wa mtoano na kilele chake kitakuwa siku ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia.

Mchezo wa ufunguzi wa  Bonanza hilo ulikuwa baina ya timu ya waendesha baiskeli kibiashara “Daladala United dhidi ya wauza mbao,ambapo  timu ya Daladala United waliwasambaratisha bila huruma timu ya Timber FC kwa mabao 5 – 3,huku Wasanii FC ikiibuka mshindi kwa kuwafunga Halmashauri S.C kwa bao 3 – 0,na Bodaboda FC waliwafungisha virago ya kushiriki Bonanza hilo timu ya Stendi United kwa kuwafunga bao 1 – 0,huku Bajaji FC wakiliaga bonanza hilo baada ya kufungwa bao 3 – 2 na Afya FC.