Thursday, June 15, 2017

RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA ‘EPL’ 2017-18,YATOKA,BINGWA MTETEZI KUANZIA NYUMBANI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



BINGWA wa Soka Uingereza msimu wa mwaka 2016/2017,timu ya Chelsea,itaanza kampeni ya kutetea taji la Ligi Kuu ya England kwa mechi ya nyumbani dhidi ya
Burnley,katika mchezo utakaochezwa mwisho wa wiki,tarehe 12-13 Agosti.mwaka huu.

Mechi ya kwanza ya Spurs katika uwanja wa Wembley itakuwa dhidi ya mabingwa wa Antonio Conte wikendi ya pili ya msimu.

Mechi za mwisho za ligi zitachezwa Jumapili 13 Mei, 2018 wiki moja mapema kuliko msimu uliopita kutokana na fainali za Kombe la Dunia ambazo zitaanza Urusi 14 Juni.
Ratiba ya mechi za Kombe la Ligi ya England itatolewa 21 Juni nayo ya mechi za Scotland siku mbili baadaye.
Mechi za ufunguzi Jumamosi, 12 Agosti, 2017
Arsenal v Leicester City
Brighton v Manchester City
Chelsea v Burnley
Crystal Palace v Huddersfield Town
Everton v Stoke City
Manchester United v West Ham United
Newcastle United v Tottenham Hotspur
Southampton v Swansea City
Watford v Liverpool
West Bromwich Albion v AFC Bournemouth

Aidha kumekuwa na mashaka kuhusu uwezo wa Tottenham kutamba Wembley ikizingatia matokeo yao katika uwanja huo Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita.

Vijana hao wa Mauricio Pochettino watakuwa an kibarua kigumu mechi yao ya kwanza uwanja huo wao wa muda.
Mara ya mwisho walipokuwa Wembley, ilikuwa nusu fainali Kombe la FA msimu uliopita ambapo walilazwa 4-2 na Chelsea.

Lakini wiki za kwanza huenda zikawa ngumu kwa mabingwa watetezi pia, huku Chelsea wakiwa wenyeji wa Everton (26 Agosti), wawatembelee washindi wa 2015-16 Leicester baada ya mapumziko ya kimataifa na kisha wawe wenyeji wa Arsenal (16 Septemba).

Vijana wa Arsene Wenger watakuwa na nafasi ya kuonyesha uwezo wao msimu ujao watakapozuru Anfield kucheza na Liverpool wiki ya tatu.
Mechi zitakazofuata Liverpool watazuru Etihad Stadium kukabiliana na Manchester City.

Katika hiyo, klabu zitacheza mechi nne katika kipindi cha siku sita wakati wa Krismasi na Mwaka Mpya, kwa jumla zitakuwa mechi nane kuanzia 2 Desemba hadi 1 Januari.
Jumamosi, 19 Agosti, 2017
AFC Bournemouth v Watford
Burnley v West Bromwich Albion
Huddersfield Town v Newcastle United
Leicester City v Brighton
Liverpool v Crystal Palace
Manchester City v Everton
Stoke City v Arsenal
Swansea City v Manchester United
Tottenham Hotspur v Chelsea
West Ham United v Southampton
Jumamosi, 26 Agosti, 2017
AFC Bournemouth v Manchester City
Chelsea v Everton
Crystal Palace v Swansea City
Huddersfield Town v Southampton
Liverpool v Arsenal
Manchester United v Leicester City
Newcastle United v West Ham United
Tottenham Hotspur v Burnley
Watford v Brighton
West Bromwich Albion

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI