IMEELEZWA zaidi ya viwanja 100, katika
eneo la Chuo cha Maendeleo ya Wananchi ( MWAMVA) kilichopo katika
Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga,vimegawiwa kwa wananchi kimakosa
na
kusababisha mgogoro mkubwa baina ya chuo na waliotwaa maeneo hayo.
Umilikishwaji huo wa Viwanja na kuibua
msigano,ni muendelezo wa maeneo ya awazi ama yanayomilikiwa na taasisi za
serikali na kidini yakiwemo makaburi,kupokwa na kufanywa vya makazi.
Akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji juzi,katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri hiyo,Anderson Msumba,alisema tatizo hilo limechangiwa na kutowajibika kwa weledi na watendaji wa Idara ya Ardhi ,watendaji wa kata pamoja na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa.
Msumaba alikiri ukosefu wa uwajibikaji unaozingatia maadili ya kazi na uliotawaliwa na maslahi binafsi imekuwa kiini cha migogoro ya Ardhi katika mji wa Kahama ambayo imekithiri na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.
Alisema
kuwepo mkwa migogoro hiyo pia kumechangia kudumaa kiuchumi kwa jamii ambayo
imekutwa ikigonganishwa katika kiwanja kimoja zaidi ya watu watatu,hivyo badala
ya wananchi hao kufanya kazi kuinua vipato vyao ambavyo huwa sababu ya kuijenga
Kahama,wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kuhudhuria mahakamani na si kujenga
Taifa.
Aidha
aliwaeleza wenyeviti hao kuwa tayari ofisi yake kwa kushirikiana na
baraza la Madiwani ameunda tume kwa ajili ya kuchunguza
migogoro hiyo na kwamba tayari imekwisha anza kazi sehemu
mbalimbali za mji huo na kuwataka wenye viti kutoa ushirikiano kwa tume hiyo
ili kutatua migogoro ya ardhi iliyopo.
Hata hivyo Msumba aliwataka wenye viti hao kutojishirikisha na suala la ugawaji wa Ardhi ili kujiepusha na migogoro baina yao na wananchi nakuongeza kuwa waendele kuwaongozi wananchi katika mitaa yao kwa kufuata misingi na kanuni za nchi bila kuvunja sheria.
Alisema
kuwa mji wa Kahama umekuwa unakuwa kwa kasi kila kukicha kutokana
na ongezeko la wageni wengi ambao wamekuwa wakiingi kwenye mji huo kwa kutaka
viwanja kwa ajili ya uwekezaji na makazi hivyo ni vyema wakaepuka kujiingiza
kwenye hali hiyo.
Kwa upande wao wenye viti hao waliahidi kushirikiana kwa pamoja na Halmashauri katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi ili Halmashauri ya mji wa Kahama iweze kusonga mbele.