Thursday, June 15, 2017

ACACIA YASALIMU AMRI,YAKUBALI KULIPA DENI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema Kampuni ya madini ya Barrick imekuabali kufanya mazungumzo na Serikali ikiwa ni pamoja na kulipa
fedha ambazo Serikali inadai kwa kufanya shughuli zake hapa nchini.

Mazungumzo hayo yamekuja baada ya Serikali kudhibiti makontena 277,yaliyoundiwa Kamati mbili za Rais,ambazo zote ziliwasilisha taarifa ambazo zilizidisha msimamo wa Serikali kudhibiti mchanga huo kutosafirishwa baada ya kubaini kampuni ya Acacia kufanya kazi kinyume cha sheria kutokana na kutokuwa na Usajili;Brela,huku ikihujumu mapato yatokanayo na usafirishaji wa mchanga wa dhahabu ( Makinikia ).

Akizungumza mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation inayomiliki kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton leo Ikulu jijini Dar es Salaama, Rais Magufuli amesema kampuni ya Barrick imekubali  mazungumzo na Serikali ya Tanzania na kulipa  fedha wanazodaiwa.

 “Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ilikufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa licha ya kampuni hiyo kukubali  kulipa fedha wanazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu  hapa nchini.

Naye, Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya  Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kulipa fedha zote ambazo inatakiwa kulipa kwa Serikali ya Tanzania.

Mazungumzo hayo kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick yalihudhuriwa na Balozi wa Canada nchini  Ian Myles na Waziri wa Katiba na sheria Prof. Palamagamba Kabudi.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI