JESHI la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya
Kahama,mkoani Shinyanga,limewataka wakazi wa mji wa Kahama,kukabiliana na
majanga ya moto kwa kumiliki
vifaa vya kudhibiti dharura hizo majumbani mwao.
Limesema jamii pindi ikijenga
utamaduni wa kuweka mitungi ya zima moto kwenye nyumba za makazi yao sambamba na sehemu za biashara zao itajinusuru na ajari za moto zinazoweza kujitokeza,na
kuwasbabishia hasara za kiuchumi,anaandika Shaban Njia.
Mkuu wa Kitengo cha Jeshi la zima moto
na uokoaji wilayani Kahama,Mkaguzi Msaidizi Frank Elophazy,ametoa ushauri huo kwa
kubainisha kwamba kuwepo kwa mitungi hiyo katika maeneo hayo, kutasaidia kudhibiti
kwa haraka viashiria vya majanga ya moto.
Meshack anasema pindi majanga ya moto
yanapojitokeza huathiri kichumi kwa kijamii inayokumbwa na kadhia hiyo,inayotokana
na uzembe wa kushindwa kuchukua hadhari
kwa kuweka mitungi ya zima moto katika nyumba zao ama sehemu mbali mbali za
biashara.
Anasema;“Wanakahama wanatakiwa kujenga
desturi ya kuweka mitungi ya zima moto katika nyumba zao,hatua itakayosaidia
kupunguza wimbi la moto,kwa kujihudumia hatua za awali kabla ya jeshi la zima
moto kufika katika eneo la tukio.”
Anabainisha kazi ya jeshi hilo
ni kufanya ukaguzi wa kina na uokozi pindi yanapotokea majanga ya moto,huku
akiikumbusha jamii kutakiwa kujenga nyumba zao kwa kufuata ramani na sheria pia
kanuni za miji,kwa kuweka miundo mbinu rafiki ya uokozi iwapo itajitokeza janga
la moto.
“Tumeweza kutoa elimu sehemu
mbalimbali juu ya matumizi ya mitungi ya zima moto katika jamii hususani
mashuleni, kwenye masoko na majumbani pamoja na sehemu za biashara,kuweza
kupunguza tatizo la ajali za moto zinapotokea,ikiwa ni pamoja na kuokoa mali
zao,” anasema Meshack.
Aidha anawasisitiza wananchi kununua
kwa wingi mitungi hiyo ya zima moto ili kuepukana na ajali za moto zisizokuwa
za lazima na kuongeza kuwa kipindi inatokea ajali ya moto wakumbuke kupiga simu
mapema ili kuokoa mali zao.
Hata hivyo anabainisha kwamba nyumba
nyingi katika wilaya ya Kahama zimejengwa bila kufuata utaratibu wa mipango
miji na kanuni zake za ujenzi hali amabayo inasababisha mali nyingi kuteketea
na moto kutokana na gari za zima moto kushindwa kuwafikia kirahisi ili kutoa
huduma hiyo ya zima moto,pindi janga la moto linapotokea.
“Tuwaombe wananchi pindi wanapotaka
kuanzisha ujenzi wa nyumba za kuishi na biashara wakitoka idara ya ardhi waweze
kufika ofisi zetu kusudi tuwape ushauri namna nyumba zao zijengwe ili kuwezesha
timu ya uokozi kutoka jeshi la zima moto kufika kirahisi na kuokoa mali,pindi
wanapokabiliwa na janga la milipuko ya moto,” anahitimisha Meshack.