MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara,Yanga African ya Jijini Dar
Es Salaam,imeangukia katika michuano ya Kombe la
Shirikisho,baada ya kushindwa
kuingia hatua ya robo fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga imeshindwa kufuzu
hatua hiyo baada ya kutoshana nguvu na timu ya Zanaco ya Zambia,ambayo imefuzu
hatua hiyo kwa faida ya bao la ugenini.
Katika
mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya mabao 1-1kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam,hivyo kutakiwa ili imudu kufuzu ni budi kutoka sare ya
mabao 2-2 na kuendelea. Au ushindi wa aina yoyote.Jambo ambalo wameshindwa
kulifanya katika uwanja wa Taifa wa Mashujaa mjini Lusaka,Zambia.
Katika pambano hilo hadi timu
zinakwenda mapumziko zilikuwa zimetoshana nguvu,pamoja na timu hizo
kushambuliana kwa zamu,lakini safu za Ulinzi kwa kila upande ulikuwa makini na
kusababisha mpira kuchezwa kati zaidi.
Dakika
ya 45 mchezo,Haji Mwinyi,alitaka
kuigharimu timu yake ya Yanga baada ya kufanya uzembe kwa kutoa pasi fupi,na
kusababisha Mlinda Mlango wake,Deogratias Munis “Dida”kufanya kazi ya ziada kuokoa
hatari hiyo.
Katika
pambano hilo,Mwamuzi kutoka nchini Kenya,aliwazawadia Kadi ya Njano wachezaji
wa Yanga;Kelvin Yondani mnamo dakika ya 37 ya mchezo,baada ya kumuangusha
Sikala na Haji Mwinyi mnamo dakika ya 75,kwa kumuangusha Musonda.