MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha,jana imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha
Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, baada ya kusota gerezani kwa zaidi
ya
miezi minne,kutokana na pingamizi lililowekwa na wakili wa serikali.
miezi minne,kutokana na pingamizi lililowekwa na wakili wa serikali.
Lema amesota kwa kipindi chote hicho kutokana na pingamizi la Wakili wa Serikali,baada ya kutuhumiwa kutoa maneno ya Kichochezi dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.a.
Hata hivyo;Mahakama
hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili
zilizowasilishwa mahakamani hapo, na kuchukua maamuzi ya kuzitupitilia mbali hoja
za upande wa serikali za kumnyima Lema dhamana.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa ni siku chache kupita tangu mahakama rufaa kutupilia
mbali rufaa ya jamhuri, huku ikishangazwa na hatua ya Lema kukosa dhama
hadi wakati huo.
Mbunge
huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili
wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1 ambapo nje ya
mahakama Lema ametoa shukrani zake kwa wote waliohusika na kubainisha
kuwa serikali haikuwa na nia njema na yeye, lakini yeye amesimama na
Mungu.
"Ninamshukuru
sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa
chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke
wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto
wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na
mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani" Amesema Lema
Kwa
upande wa wakili wake Peter Kibatala amesema hatimaye kazi ya kwanza ya
kuhakikisha Lema anapata dhamana imekamilika na kwamba sasa wanajipanga
kwa ajili ya kushughulika na kesi ya msingi.
Kwa
niaba ya CHADEMA, Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, amelaani nguvu
iliyotumiwa na jeshi la polisi,mahakamani hapo kuwapiga, kuwakamata na
kuwatawanya wafuasi wa chama hicho waliofika mahakamani hapo kufuatilia
kesi ya mbunge wao, huku akitangaza hakutakuwa na tukio
lolote la kisiasa mpaka watakapotangaziwa tena.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI